Na Benny Mwaipaja-WFM, Dodoma

SERIKALI imeendelea kupata neema kutokana na uwekezaji wake kwenye mashirika na taasisi mbalimbali yanayojiendesha kibiashara nchini ambapo leo Shirika la Bima la Taifa (NIC) limetoa gawiwo la Shilingi bilioni 1.707 baada ya kupata faida kiabishara mwaka 2016/2017.

Kwa nyakati tofauti mwaka huu, Serikali ilipokea kiasi cha Shilingi bilioni 1.7 kutoka Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) na kufuatiwa na NMB Bank Plc, iliyotoa kiasi cha Shilingi bilioni 16.5 hivi karibuni.

Akipokea Hundi kifani ya kiasi hicho cha Shilingi 1.707 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa, Bw. Sam Kamanga, Waziri wa Fedha na Mipango, amelipongeza shirika hilo kwa kuonesha maendeleo makubwa katika kipindi kifupi tangu azindue Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika hilo mwishoni mwa mwaka uliopita.

“Nilipozindua Bodi yenu ya Wakurugenzi uliniahidi Mkurugenzi Mtendaji kuwa mtafanyakazi kwa bidii na kuanza kutoa gawiwo Serikalini, ninajisikia furaha sana kwa niaba ya watanzania kuona kuwa mnatimiza ahadi hiyo kwa kutoa asilimia 15 ya pato ghafi la mapato yenu. Nawapongezeni sana” alisisitiza Dkt. Mpango.

Alizitaka taasisi nyingine za umma zilizochini ya Ofisi ya Msajili wa Hazina zinazofikia 260 kuanza kutumia huduma za bima kupitia Shirika la Bima la Taifa.

CHEKI
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Bw. Sam Kamanga akimkabidhi Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), Hundi kifani yenye thamani ya  Sh. bil. 1,707,900,000, ambazo ni gawiwo ambalo Serikali imepata baada ya Shirika hilo kupata faida kwa mwaka wa fedha 2016/2017, Makao Makuu ya Wizara Mjini Dodoma.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Bw. Sam Kamanga, akizungumza jambo wakati wa tukio la Shirika hilo kukabidhi gawiwo kwa Serikali, kiasi cha Sh. Bil. 1.7, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha, mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (MB) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Bw. Sam Kamanga, katika hafla ya makabidhiano ya gawiwo la Sh. Bil.1.7 liyofanyika mjini Dodoma.
Viongozi waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango, wakishiriki tukio la Shirika la Bima la Taifa (NIC) kuikabidhi Serikali gawiwo la Sh. Bil. 1.7 baada ya Shirika hilo kufanya vizuri kibiashara katika Mwaka wa Fedha 2016/2017, tukio lililofanyika makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, mjini Dodom
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Doroth Mwanyika, akifurahia jambo wakati wa tukio la Shirika la Bima la Taifa (NIC) kuikabidhi Serikali gawiwo la Sh. Bil. 1.7 baada ya Shirika hilo kupata faida katika mwaka wa fedha 2016/2017
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akisisitiza jambo wakati wa tukio la Shirika la Bima la Taifa (NIC) kukabidhi Serikalini gawiwo la Sh. bil. 1.7, baada ya Shirika hilo kupata faida kibiashara katika mwaka wa Fedha 2016/2017, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango Mjini Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, akitoa neno la Shukrani kwa uongozi Shirika la Bima la Taifa (NIC) kwa ubunifu na uwajibikaji wao ulioliwezesha Shirika hilo kupata faida na kutoa gawiwo kwa Serikali, Mjini Dodoma.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...