Katika kutekeleza Sera ya Diplomasia ya Uchumi, Ubalozi wa Tanzania kwa kushirikiana na Ubalozi wa Uholanzi uliopo Tanzania, Wizara ya Masuala ya Uchumi na Wizara ya Mambo ya Nje za Uholanzi na Taasisi ya Netherlands–African Business Council (NABC)kwa pamoja ziliandaa Kongamano la Biashara na Uwekezaji lililofanyika hapa The Hague, Uholanzi tarehe 31 Mei 2017. 

Lengo kuu la Kongamamo hilo, pamoja na kuendeleza na kukuza uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Uholanzi, nikutangaza fursa mbalimbali za biashara na uwekezaji zilizopo nchini Tanzania hususan katika Sekta za Kilimo, Ufugaji, Uvuvi na Miundombinu ya Kilimo. 

Aidha, Kongamano hilo lililohudhuriwa na Wawakilishi wa Makampuni takriban mia moja (100) ni mwendelezo wa utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa kwenye Mkataba kati ya Tanzania na Uholanzi kuhusu Uingizwaji wa Mbegu za Viazi kutoka Uholanzi uliosainiwa kwenye ziara ya Mhe. Martijn Van Dam, Waziri wa Kilimo wa Uholanzi nchini Tanzania tarehe 16 Juni 2016. 

Aidha, Kongamano hii lilitanguliwa na ziara ya ujumbe kutembelea maeneo mbalimbali ikiwemo mashamba yanayomilikiwa na wakulima na wafugaji binafsi nchini Tanzania pamoja na kupata fursa za kusikiliza mada mbalimbali zilizotolewa na wakulima/wafugaji na wakufunzi wa Chuo Kikuu cha Wageningen kinachohusika na kufanya tafiti za Kilimo na Ufugaji.

Ujumbe kutoka Tanzania uliongozwa na Mhe.Eng. Mathew Mtigumwe, Katibu Mkuu anayeshughulikia Kilimo kutoka Wizara ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi, akimwakilisha Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

Uwekaji saini wa makubaliano (letter of intent) ya kuanzishwa kwa kituo cha kuendeleza zao la viazi Tanzania .
Picha ya Pamoja ya Waheshimiwa Mabalozi wa Tanzania na Uhoalnzi na Makatibu Wakuu wa Kilimo na Uvuvi na Mkurugenzi wa TAHA. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...