Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi kote nchi kuwafichua watu wanaonyanyasa na kudhalilisha watoto kijinsia ili waweze kukamatwa na kuchukua hatua za kisheria kama hatua ya kukomesha vitendo hivyo ambayo vimeanza kushamiri katika baadhi ya jamii nchini.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa agizo hilo katika hotuba yake ya kuhitimisha kampeni ya kudhibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambayo ilitoa huduma bure za vipimo na matibabu kwa watoto na vijana zaidi ya 1500 kampeni ambayo iliambatana na maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika katika viwanja vya Shule ya msingi Kinyerezi mkoani Dar es Salaam.

Makamu wa Rais amesema kuwa watenda maovu hao lazima vifichuliwe na wananchi, walezi pamoja na wazazi kwa kuwa watu wanaofanya vitendo hivyo vya udhalilishaji wa watoto wapo miongoni mwa jamii.

Katika kukabiliana na hali hiyo, Makamu wa Rais ameviagiza vyombo vya dola kutofumbua macho vitendo hivyo bali pindi wanapopata taarifa za matukio ya udhalilishaji wa watoto wachukue hatua za haraka za kuwakamata na kuwachukulia hatua stahiki watu wanaofanya vitendo hivyo vibaya.

Makamu wa Rais pia ametoa wito maalum kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kote nchini waache kuwaficha watu wanaotendea vitendo hivyo vibaya bali wawapatie taarifa walimu wao na polisi ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Amesema kwa kufanya hivyo watoto watakuwa salama katika mazingira ya nyumbani na wakiwa mashuleni kwani watu wabaya wanaofanya vitendo hivyo watawajibishwa kulingana na matendo maovu waliyokuwa wanawafanyia watoto hao.

“Mtoto anaweza kufaidika na fursa sawa iwapo tu atalindwa kwa kuwezeshwa kuwa afya bora”, Amesisitiza Makamu wa Rais.

Kuhusu kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema magonjwa yasiyo ya kuambukiza yameendelea kuua watu kwa kasi katika nchi zinazoendelea Kusini mwa Jangwa la Sahara ikiwemo Tanzania.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akihutubia kwenye Tamasha la Uelimishaji na Upimaji Afya na Kinga dhidi ya Magonjwa yasiyoambukiza kwa watoto na vijana kwenye uwanja wa michezo wa shule ya msingi Kinyerezi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiteta jambo na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla wakati Tamasha la Uelimishaji na Upimaji Afya na Kinga dhidi ya Magonjwa yasiyoambukiza kwa watoto na vijana kwenye uwanja wa michezo wa shule ya msingi Kinyerezi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Meza Kuu Ifurahia Jambo.
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwaaga wageni mbalimbali waliofika kwenye Tamasha la Uelimishaji na Upimaji Afya na Kinga dhidi ya Magonjwa yasiyoambukiza kwa watoto na vijana kwenye uwanja wa michezo wa shule ya msingi Kinyerezi. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Mhe.Sophia Mjema
Burudani mbalimbali zilitolewa kwenye tamasha hilo 



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...