Na Humphrey
Shao,Globu ya Jamii
Kampuni ya
uuzaji wa vifaa vya Michezo ya ,Speshoz Tanzania imeingia mkataba wa kutoa
vifaa vya Michezo kwa timu ya Soka ya Lipuli ya Iringa ambayo imepanda kucheza ligi
kuu ya Vodacom Tanzania.
Akizungumza
wakati wa kusaini mkataba wa timu hiyo mkurugenzi wa Speshoz Tanzania,Jeffrey
Jessey amesema mkataba huo ambao ni wa zaidi ya Milioni 30 utawawezesha kuuza
jezi za Lipuli na kuwagawia vifaa vyote vya mazoezi.
“mkataba huu
utaweza kuisadia timu hii kuwa na vifaa vya uhakika na vya kisasa ambavyo
vitasaidia timu hiyo kuwa na morali na kuhimili ushindani na timu mkubwa”
Amesema Jessey.
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa timu ya Lipuli, Abu Changawa amesema kuwa mkataba huo ni
moja ya vitu ambavyo vitasaidia timu hiyo kuwa na vifaa vya uhakika.
Amesema kuwa
kampuni hiyo imewapa masharti kuwa timu hiyo ikifanikiwa kubaki sita bora basi
wataongeza udhamini katika msimu ujao.
Changawa
amesema ni vyema makampuni mengine yakajitokeza kusaidia timu hiyo kwa upande
wa udhamini hili iweze kufanya vizuri.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Speshoz Tanzania Jeffrey Jessey akizungumza na Waandishi wa habari juu ya Mkataba wake na timu ya soka ya Lipuli ya Mkoani Iringa
Mkurugenzi wa Kampuni ya Speshoz Tanzania ,Jeffrey Jessey na Mwenyekiti wa Lipuli Abu Changawa wakisaini Mkataba wa Vifaa vya Michezo
Mkurugenzi wa Kampuni ya Speshoz Tanzania ,Jeffrey Jessey na Mwenyekiti wa Lipuli Abu Changawa wakipeana mikono baada ya kusaini Mkataba wa Vifaa vya Michezo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...