Madiwani wanawake wa vyama mbalimbali vya siasa katika Mkoa wa Dar es Salaam wamesema suala la kubadili mtazamo katika ushirikishwaji wa wanawake kwenye maendeleo ni la msingi na linapaswa kutekelezwa kuanzia ngazi za chini. 


Wakizungumza katika warsha ya siku tatu ya Uongozi wa Kijinsia iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP Mtandao), madiwani hao wamesema haki za wanawake bado zinakandamizwa katika jamii huku vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia vikishika kasi. 


Akizungumza katika mafunzo ya siku tatu Spika Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Anne Makinda amesema wanawake wanapaswa kuungana kwa pamoja wanapokuwa wanapigania haki zao za msingi. Amewasisitiza kuachana na masuala ya vyama kwenye jambo linalowahusu wanawake wote. Wakifanya hivyo wataweza kupunguza tabaka kubwa kwenye utawala na hata kwenye uzalishaji mali.
Spika Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Anne Makinda akiwahamasisha Madiwani wanawake wa Jiji la Dar es Salaam walioudhuria mafunzo  ya uongozi, jinsia na bajeti yenye mlengo wa kijinsia pamoja na kutoa uzoefu wake kwenye maswala ya uongozi  kwa wanawake hasa ngazi za juu leo kwenye ukumbi wa TGNP Mtandano jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi Lilian Liundi akizungumza na Madiwani Wanawake kuhusu nguvu ya mwanamke kwenye  jamii  pamoja na kuwapa miongozo kuhusu nafasi zao kwenye uongozi ili kufikia lengo la hamsini kwa hamsini.

Mwanachama wa TGNP Mtandao na mkufunzi wa Mafunzo ya Madiwani wanawake wa Jiji la Dar Es Salaam Profesa Ruth Meena akiwasilisha  mada kuhusu kujitambua kwa mwanamke kwenye jamii, kujua thamani yake pamoja na mchango wake kwenye jamii katika mafunzo yaliyofanyika kwenye ukumbiwa TGNP Mtandao jijini Dar es Salaam.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...