Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akipokea Barua ya kujitambulisha na kuomba msaada wa mchango kwa ajili ya kufanya Mkutano Mkuu wa Chama cha Askari wastaafu kwa Vita kuu ya pili ya dunia waliopigana Mwaka 1939 – 1945 kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama hicho ambae ni Ndg. Bakari Ngonja, katika kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akutana na kufanya mazungumzo na Chama cha Askari wastaafu wa Vita kuu ya pili ya dunia waliopigana Mwaka 1939 -1945 katika kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akisisitiza jambo pale alipokutana na kufanya mazungumzo na Chama cha Askari wastaafu wa Vita kuu ya pili ya dunia waliopigana Mwaka 1939 -1945 katika kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma. (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mheshimiwa Mkuu wa wilaya ya Nanihii,
    Hili neno "vita" katika kiswahili liko kwenye ngeli ipi?
    Sikubali liko kwenye ngeli ya i-zi.
    (Naamini unaelewa nnachozungumza)
    Kwa uelewa wangu wa lugha ya Kiswahili, neno vita liwe "vita vya" na wala siyo "vita ya".
    Tatizo la Kiswahili ni kutumiwa vibaya na watumizi wakubwa kama vile wanasiasa wetu ambao lugha hii si ya kwanza kwao.
    Wanapoipotosha, na kwa kuwa wao ndio sauti zao hupazwa, na kwa kuwa hata wanahabari wetu karibu woote hawana shahada za lugha ya Kiswahili, matokeo yake lugha yetu adhimu inavurugika.
    Kwa kuwa mmeamua Kiswahili kiwe lugha ya matumizi, liwrkwe sharti kuwa kila mwanasiasa na mwanahabari aingie darasani kukisoma.
    Kuanzia sasa msiseme vita kuu ya pili ila mseme vita vikuu vya pili.
    Sawasawa?
    Shukrani globu ya jamii.
    Mndengereko, Ukerewe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...