THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Swala ya eid El fitri kufanyika siku ya jumatatu viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar - Alhad Mussa Salum

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhad Mussa Salum amewatangazia waumini wa dini ya kiislam kuwa Swala ya eid El fitri itaswaliwa mnamo siku ya jumatatu Juni 26, 2017 katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam, ikiwa ni baada ya kukamilika mfungo mtukufu wa mwezi wa Ramadhani.

Sheikh Salum aliyazungumza hayo jana wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari, na amewataka na kuwaasa waumini wa kiislam kuhakikisha wanatekeleza mema yote kama waliyokuwa wakiyafanya katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Akizungumzia siku ya ibada hiyo muhimu kwa waislam wote ulimwenguni, Sheikh Salum alimesema katika viwanja vya mnazi wageni mbali mbali wanatarajiwa kuwepo, lakini pia mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ali Hassan Mwinyi.


Hoja moja imeshachangiwa mpaka sasa.

  1. konaball Anasema:

    Ana uhakika gani kama mwezi hautoandama mwezi 29??