MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), imejivunia kujenga shule ya kisasa ya msingi ya Tumaini iliyopo kata ya Mafumbo, wilaya ya Bukoba Mjini ili iwe mbadala wa shule ya Tumaini iliyopo eneo la karibu na uzio wa Kiwanja cha ndege.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Bw. Salim Msangi amesema shule hiyo inamajengo tisa yenye madarasa 24 kati ya hayo 21 ni ya watoto wasio na mahitaji maalum na matatu ni ya watoto wenye mahitaji maalum; zipo ofisi za walimu, vyoo vya shule na vya walimu, na nyumba ya kukaa mwalimu mmoja.

“Ninaona fahari kubwa na nimefarijika sana kuona shule imekamilika kwa kiwango kikubwa na sasa watoto wetu watasoma katika mazingira ya ya utulivu na amani tofauti na awali katika shule ya Tumaini kulikuwa na kelele za ndege kila zinapotua na zinaporuka,” amesema bw. Msangi.

Pia Bw. Msangi amesema shule ya zamani ilikuwa katika maeneo hatarishi ya karibu na barabara ya kutua na kuruka kwa ndege, jambo ambalo lingeweza kuleta maafa makubwa endapo kungetokea ajali maeneo hayo.

Naye mkandarasi wa mradi huo kutoka kampuni ya ujenzi ya CMG ya Mwanza, Mhandisi Jumanne Warema amesema pia madarasa hayo yatawekewa madawadi 315, meza na viti 16 za walimu na madarasa ya watoto wenye mahitaji yatawekwa viti maalumu 48.

Mkuu wa shule ya Tumaini, Bw. Theophil Ndyakowa ameishukuru TAA kwa msaada huo mkubwa walioutoa kwa ujenzi wa shule ya kisasa, ambapo sasa wanafunzi watasoma kwa bidii zaidi.

Hata hivyo mradi huo wa shule umedhaminiwa na Benki ya Dunia, ambapo pia wamefanikisha ujenzi wa jengo la kisasa la abiria, jengo la kuhifadhi umeme na kukarabati barabara ya kutua na kuruka kwa ndege.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Dr. Leonard Chamuriho (watatu kushoto) akiwafafanulia jambo wahandisi Diana Munubi na Mbila Mdemu (kushoto) huku Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Salim Msangi (mwenye suti nyeusi) akisikiliza mara baada ya kukagua shule mpya ya msingi ya kisasa ya Tumaini iliyopo Bukoba.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Salim Msangi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto wa shule ya kisasa ya msingi ya Tumaini iliyopo kata ya Mafumbo, wilaya ya Bukoba Mjini.
Wanafunzi waliohamishiwa kutoka katika shule ya msingi Tumaini iliyokuwa maeneo ya karibu na kiwanja cha ndege cha Bukoba, sasa wakiwa mapumziko kwenye shule mpya iliyojengwa maeneo ya Mafumbo kwa usimamizi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...