Kipa Aishi Manula, akichupa kudaka mpira wakati wa mazoezi yanayosimamiwa na Kocha wa Makipa wa Taifa Stars, Patrick Mwangata aliyepiga magoti katika mazoezi yanayofanyika Kituo cha michezo cha Tolip (Tolip Sports City) hapa Alexandria, Misri. Taifa Stars  inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti inayozalishwa na Kampuni ya Bia ya SBL, inajiandaa kucheza na Lesotho Juni 10, 2017 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika Cameroon. 
 Kipa Said Mohammed Nduda , akichupa kuzuia mpira wakati wa mazoezi yanayosimamiwa na Kocha wa Makipa wa Taifa Stars, Patrick Mwangata aliyepiga magoti katika mazoezi yanayofanyika Kituo cha michezo cha Tolip (Tolip Sports City) hapa Alexandria, Misri. 
 Kipa Benno Kakolanya, akidaka mpira wakati wa mazoezi yanayosimamiwa na Kocha wa Makipa wa Taifa Stars, Patrick Mwangata aliyepiga magoti katika mazoezi yanayofanyika Kituo cha michezo cha Tolip (Tolip Sports City) hapa Alexandria, Misri. 
 Kiungo wa pembeni wa Taifa Stars, Simon Msuva akiwa kwenye kasi kuwahi mpira wakati wa mazoezi ya timu hiyo yanayofanyika Kituo cha michezo cha Tolip (Tolip Sports City) hapa Alexandria, Misri. 
Libero wa Taifa Stars, Erasto Nyoni (katikati) akijitahidi kudhibiti mpira mbele ya washambuliaji wenye njaa ya kufunga, Ibrahim Ajib (kulia) na Abderheman Mussa kabla ya kipa Said Mohammed hajatokea kusaidia wakati wa mazoezi ya timu hiyo yanayofanyika Kituo cha michezo cha Tolip (Tolip Sports City) hapa Alexandria, Misri.  Picha na Alfred Lucas wa TFF.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...