Taifa Stars - Picha na Bin Zubeiry
Timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti, itaingia kambini tena Juni 14, mwaka huu kujiandaa na michuano inayoratibiwa na Baraza la Soka la Kusini mwa Afrika (COSAFA).
Michuano hiyo inatarajiwa kuanza Juni 25, mwaka huu ambako Taifa Stars itakwenda Afrika Kusini, Juni 20, mwaka huu.Kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga amepanga kufanya mabadiliko madogo ya kikosi cha Taifa Stars kitakaochokwenda kushiriki michuano hiyo.
Kocha kesho atafanya uteuzi wa wachezaji wengine atakaowajumuisha kwenye kikosi chake, atafanya mabadiliko kidogo hivyo  kesho atatangaza majina ya wachezaji ambao wataingia kambini kujiandaa na michuano hii ya Cosafa inayoanza Juni 25 huko Afrika Kusini.
Wakati huo huo, awamu ya pili ya kozi ya Daraja A inayoendeshwa na Shirikisho la soka Afrika (CAF) imeanza leo kwenye ukumbi wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF).Kozi hiyo inahusisha makocha 20 ambao walishiriki kwenye kozi hiyo ya awamu ya kwanza iliyofanyika jijini Dar es Salaam Novemba, mwaka jana.
Mkufunzi wa kozi hiyo ni Mtanzania Sunday Kayuni ambaye pia atakuwa na wataalam wa masuala ya Lishe, Masoko, Tiba, Habari, Bima pamoja na mtaalam wa masuala ya upingaji wa matumizi ya utumiaji wa dawa  kuongeza nguvu michezoni.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...