Kiwanda cha Kuzalisha Viuadudu vya Kuua Viluwiluwi vya Mbu wa Malaria kilichopo Kibaha, Mkoani Pwani.
Tarehe 22 June 2017, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alilipia VIUADUDU vya kutokomeza Mbu wa Malaria lita 100,000 na kuagiza vigawanywe kwenye Halmashauri zote nchini.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu anapenda kuwatanganzia Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuwa VIUADUDU hivi vitaanza kugawiwa leo kwa Halmashauri za Mikoa 14 yenye kiwango kikubwa cha Maambukizi ya Ugonjwa wa Malaria. 

Mikoa hii (na kiwango cha maambukizi ya malaria kimeonyeshwa kwenye mabano) ni;- Kagera (41%), Geita (38%), Kigoma (38%), Ruvuma (23%), Tabora (20%), Mtwara (20%), Mara (19%), Morogoro (14%), Shinyanga (17%), Lindi (17%), Pwani (15%), Mwanza (15%), Katavi (14%) na Simiyu (13%).

Mikoa mingine ambayo haijatajwa itagawia Viuadudu katika Awamu ijayo. Idadi ya Lita zitakazogawanywa kwa kila Halmashauri zilizo katika Mikoa  hii tayari imeshaainishwa.

Wizara inawakumbusha Waganga Wakuu wa Mikoa/Wilaya kufanya Upuliziaji wa Viuadudu kwa kuzingatia Miongozo ya Wizara ya Afya. Hii itawezesha kupata matokeo tarajiwa ya kutokomeza mbu ili kudhibiti ugonjwa wa Malaria nchini. 
Aidha, Wizara ya Afya inapenda kumshukuru kwa dhati na kumpongeza Mhe.Rais Dkt. Magufuli kwa kuongeza chachu katika Mapambano dhidi ya Malaria Nchini. 

Imetolewa na;
Catherine Sungura
Kaimu Msemaji- Idara Kuu  Afya
26 June 2017

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...