ESTER NAPENDA MFINANGA
(1952 – 2017)


Kwa niaba ya wanandugu wote Ndugu Boniface A. Mfinanga wa Chanjale, Kisangara Mwanga Kilimanjaro anayo heshima kubwa kutoa shukrani za dhati kabisa kwa ndugu, jamaa na marafiki ambao walishiriki kwa namna moja au nyingine katika kufanikisha mazishi ya mama yao mpendwa, ESTER NAPENDA MFINANGA aliyefariki dunia siku ya tarehe 13/4/2017 Neema Roman Catholic Health Centre Mwanga na kuzikwa kijijini kwao Chanjale, Kisangara, Mwanga, Kilimanjaro tarehe 17/4/2017

Kwa vile mlioungana nasi kwa kutufariji wakati wa kipindi chote cha msiba huu mkubwa ni wengi na ni vigumu kuwataja wote kwa majina, kama familia tunapenda kwa heshima kubwa kutoa shukrani za jumla tukiwaomba wote mkubali kuzipokea kwa moyo ule ule kama mlivyotuunga mkono. Mmetufariji sana, mmekesha nasi, mmeshinda nasi, nyote mmekuwa kimbilio salama kwetu wakati wa kipindi hiki kigumu. Mlionyesha upendo wa kweli kwetu kama familia na kwa mama yetu mpendwa.


Tunapenda kutoa shukurani za kipekee kwa  marafiki na wanandugu ambao michango yao itabakia kwa familia na nyoyo za watoto wa marehemu tukianza na Ndugu wote, majirani na marafiki wa karibu  kutoka Mwanga, Kisangara, Lembeni, Kifaru, Kiruru, Kilomeni, Soffe, Kisangara juu, Same, Pongwe Tanga, Bukoba, Moshi, Arusha, Mwanza na Dar es Salaam, kweli michango yenu kamwe haitasahaulika.



Familia pia inapenda kuwashukuru Baba askofu mstahafu Jacob Koda, Baba Paroko wa Parokia ya Chanjale Samwel Lawena, Padre Peter Mvungi, Padre Valence Sewangi, na Padre Anthony Mmari kwa kutuongozea misa takatifu ya kumpumzisha mama yetu mpendwa katika nyumba yake ya milele.

Familia vile vile inapenda kutoa shukrani za dhati kabisa kwa Dr Avelin Kimario na  Dr Swai  pamoja na manesi Prisca Silayo, Prediganda Kimario, Lightness Mduma, Donatila Msuya na Vaileth Mdee  wa NEEMA ROMAN CATHOLIC HEALTH CENTRE Mwanga, Kilimanjaro  kwa juhudi zao za dhati kabisa za kutaka kuokoa maisha ya mama yetu mpendwa.


Aidha, tunatoa shukrani kwa wafanyakazi na uongozi wa TANAPA Arusha, MSD Tanga na Bukoba, South African High Commission Dar es Salaam Mission, Murhandzwa Ltd, Tanganyika Arms Ltd, Ndugu Marwa Issa wa Kiliflora Ltd, Ndugu Gabin Msuya na wafanyakazi wote wa MSUYA AUTO GARAGE Mwanga, Wanajumuiya wa Mashahidi wa Uganda kanisa la Kristo Mfalme Moshi, Wanajumuiya ya Mt. Petro parokia ya Mwanga, Magrooup yote ya WhatsApp ya wanandugu na marafiki kwa michango yenu  iliyotufariji, tutaendelea kukumbuka ukarimu wenu daima. 


Vile vile familia inawashukuru sana majirani wa Mwanga, Chanjale, Kisangara kwa kushiriki na kushughulika kwa heshima zote katika msiba wa Mama yetu mpendwa.


Mwisho Tunawashukuru wote mlioweza kufika nyumbani Chanjale, Kisangara Mwanga na kumhifadhi Mama yetu mpendwa ESTER NAPENDA MFINANGA katika nyumba yake ya milele. Hatuna cha kuwalipa, Mungu atawalipa zaidi na zaidi.


Mama utakumbukwa daima na wanafamilia wote, Kaka na dada zako, shangazi, na wanao woote hususani Boniface, Bona, Yukunda, Bruno, Dorice, Luciana, Anastazia (Team Napenda) na wajukuu wako woote hususani Nice, Ester, Anatoly, Primi, Laris na Emmilyne

Quotes from Mom
1. “MUWASAMEHE MADHAMBI YAO NA MUWAPENDE”
                               2. “MGURANE”

BWANA ALITOA BWANA AMETWAA, JINA LA BWANA LIHIMIDIWE
AMEN


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...