Na Estom Sanga-TASAF

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF- umeibuka mshindi wa kwanza kati ya Mifuko 19 inayojihusisha na shughuli za kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa mwaka 2017 nchini.

Ushindi huo umetangazwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi –NEEC- baada ya tathimini ya kutambua mchango wa Mifuko hiyo iliyoanzishwa na serikali kwa lengo la kupunguza changamoto ya upatikanaji wa mitaji kwa wananchi hususani wale wa kipato cha chini ili waweze kuboresha maisha yao.

Taarifa iliyotolewa na NEEC imeonyesha kuwa TASAF imepata alama 81 ikifuatiwa na Mfuko wa SELF Microfinance uliopata alama 71 huku Mfuko wa Kuwaendeleza Wajasiliamali Wananchi NEDF ukipata alama 70 na kushika alama ya tatu.

Miongoni mwa vigezo vilivyoupa ushindi Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF ni pamoja na Idadi kubwa ya wanufaika wa huduma zake kutoka Kaya zipatazo MILIONI MOJA NA LAKI MOJA ,uwezo wake wa kuwafikia walengwa nchini kote,thamani ya fedha zilizowanufaisha walengwa na uwasilishaji wa taarifa za utekelezaji wa shughuli zake kwa wakati.

Akizungumza na Wafanyakazi kufuatia ushindi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga amewahimiza waendelee kujituma zaidi katika utendaji kazi,ili mchango wao katika vita dhidi ya umasikini uwe endelevu na wenye kutoa tija kwa taifa.

Bwana Mwamanga amesema ni vema wakati wote wa utekelezaji wa shughuli , watumishi wa TASAF waendelee kuzingatia maadili bora ya utumishi wa umma, na kuwapa huduma stahiki wananchi na kutekelezaji maagizo ya serikali ya uboreshaji wa huduma kwa wananchi ili kuwapunguzia kero ya umasikini.

  Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge ,Kazi, Vijana na Walemavu Mhe. Jennista Mhagama akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Bwana Ladislaus Mwamanga Cheti cha Ushindi wa Kwanza katika ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi nchini.


 Baadhi ya wafanyakazi wa TASAF wakifurahia ushindi wa kwanza ambao Mfuko huo umepata kwa mwaka 2017 kati ya mifuko 19 inayoshughulikia uwezeshaji wananchi kiuchumi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...