Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
Tatizo
la ugonjwa wa macho katika nchi ni kubwa ambalo linachangiwa kwa
kukosa rasilimali watu pamoja na vifaa vya kisasa katika kutatua
changamoto hiyo.
Akizungumza
katika kikao cha wadau wanaoshughulika na masuala ya macho
kilichoandaliwa na Sightsavers , Kaimu Meneja wa Mpango wa Taifa wa
Huduma za Macho wa Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii , Jinsia , Wazee
na Watoto, Dk. Bernadetha Shilio amesema tatizo la macho ni dogo katika
nchi lakini kutokana na kukosa kwa rasilimali watu pamoja na vifaa vya
kufanyia oparesheni linafanya tatizo kuwa kubwa.
Amesema
kutokana na tatizo la ugonjwa wa macho kuwa kubwa wameandaa mikakati ya
kutatua,ikiwemo kuongeza rasilimali watu pamoja na vitendea kazi kwa
ajili ya kufanyia operesheni.
Dkt.Bernadetha
amesema kuwa kuna ushirikiano na mashirika mbalimbali katika
yanayosaidia kutoa huduma ya ugonjwa wa macho katika sehemu mbalimbali
nchini.Mkurugenzi Mkazi wa Sightsavers, Gosbart Katuzi amesema kuwa
tatizo la ugonjwa wa macho unatokana na kitoto cha jicho na kufanya
wengine kupofoka.
Amesema
kuwa katika mradi mwaka 2009 walipeleka vifaa katika mkoa morogoro
ambapo katika kliniki hiyo zaidi watu 12000 walibainika kuwa na ugonjwa
wa macho.Katuzi amesema kuwa kwa sasa ya watu milioni moja wana matatizo
ya macho hali hiyo jitihada zinatakiwa kufanyika katika kuifikia idadi
hiyo ambayo itakuwa ikiongezeka kwa kila mwaka.
Mkurugenzi
wa Help Age International, Smart Daniel amesema ugonjwa wa macho
umekuwa ukiwakumba wazee ambapo hushindwa kufanya kazi zao kutokana na
ugonjwa wa macho.
Amesema
kuwa kuna jitihada ambazo zimekuwa zikifanyika katika kuwafikia wenye
ugonjwa macho na watu wengine kwa kufanyiwa oparesheni.
Kaimu
Meneja wa Mapngo wa Taifa wa Huduma za Macho wa Wizara ya Afya ,
Maendeleo ya Jamii , Jinsia , Wazee na Watoto, Dk. Bernadetha Shilio
akizungumza katika kikao juu wadau wanashughulika na ugonjwa wa macho
leo jijini Dar es Salaam.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Sightsavers, Caroline Harper akizungumza juu ya
taasisi hiyo ilivyoweza kusaidia maeneo mbalimbali nchini kwa watu wenye
ugonjwa macho leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Help Age International, Smart Daniel akizungumza katika mkutano wa
wadau wanaoshughulika na ugonjwa macho juu ya wazee walivyokuwa wahanga
wa ugonjwa huo leo jijini Dar es Salaam.
Afisa
Mahusiano na Masoko wa Standard Chartered ,Juanita Mramba akizungumza
juu ya utoaji wa msaada wa benki hiyo kwa watu wenye ugonjwa wa macho
leo jijini Dar es Salaam
Wadau wa wanaoshulika na ugonjwa wa macho wakiwa katika picha pamoja leo jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...