Na Richard Mwaikenda

MAFUNZO ya kujiamini na kujitambua kwa mtoto wa kike yamepamba moto katika kambi maalumu inayoendelea eneo la Mombasa, Ilala, Dar es Salaam.

Kambi hiyo iliyoandaliwa na Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), inashirikisha walimu na viongozi wa chama hicho kutoka mikoa mbalimbali nchini.

Akizungumza na mwandishi wetu aliyetembelea kambi hiyo leo,Kamishna wa TGGA,Mkoa wa Tanga, Modesta Mshata alisema kuwa lengo la kambi hiyo ni kuwajengea uwezo walimu na viongozi wa kujiamini na kujitambua.

"Tunata mtoto wa kike popote alipo ajiamini, ajitambue na kuwa jasiri ikiwemo pia kumudu maisha kwa kushirikiana vyema na jamii inayomzunguka."Alisema Mshata.

Pia alisema kuwa, lengo ni kumfundisha mtoto wa kike kuwa mama na kiongozi bora wa familia na taifa kwa ujumla. Washiriki 36 wa kambi hiyo ya siku tano wanatoka Kondoa, Dodoma, Tanga, Lindi, Rukwa na Dar es Salaam pamoja na nchi za Uganda, Rwanda na Madagascar.

Washiriki wa Kambi ya Mafunzo ya kuwajengea uwezo wanawake wakiimba  wimbo wa Taifa baada ya kujifunza jinsi ya kufunga kamba vifundo na kupandisha bendera ya Taifa katika kambi ya siku tano iliyoandaliwa na Tanzania Girl Guides Association (TGGA), Mombasa, Dar es Salaam
Wakiimba wimbo wa Taifa

Walimu na viongozi wa chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), wakijenga mahema kwa ajili ya kambi ya kumjengea uwezo mtoto wa kike yaliyoandaliwa na TGGA, Mombasa, Dar es Salaam jana. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

Wakijifunza kufunga vifundo kwenye mti.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...