Chuo Cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kwa mara ya kwanza kimeanzisha Masomo ya Shahada ya kwanza (Degree) katika fani za Uhazili na Utunzaji wa Kumbukumbu, Taarifa na Nyaraka.

Kufuatia kuanzishwa kwa masomo ya Shahada ya kwanza katika Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Mkuu wa Chuo Dkt. Henry Mambo ametoa wito kwa watumishi wa umma na Watanzania wenye sifa kuchangamkia nafasi hizo za masomo kwa manufaa yao binafsi na Taifa kwa ujumla.

Dkt. Mambo alisema masomo hayo ya Shahada ya kwanza yataanza Mwezi Septemba,2017 katika Matawi ya Dar es Salaam na Tabora, nayo ni hatua kubwa kwa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania katika kuwaendeleza Watumishi na Watanzania Kitaaluma.

Kwa upande wa sifa za kujiunga na masomo hayo ya shahada ya kwanza, Dkt. Mambo alisema muombaji anatakiwa kuwa na elimu ya kidato cha sita pamoja na ufaulu katika masomo mawili au Diploma katika fani husika yenye ufaulu au GPA alama 3.

Mkuu wa Chuo pia aliendelea kufafanua kwamba Masomo hayo ya ngazi ya Shahada yameanzishwa ili kuhakikisha kwamba watumishi wa umma na Watanzania wenye sifa za kujiunga wanakabiliana na changamoto zinazojitokeza katika soko la ajira kufuatia mabadiliko ya teknolojia na mifumo mbalimbali ya utendaji kazi.“Kutokana na mabadiliko hayo ni vema Watumishi wa Umma na Watanzania wenye sifa kwa ujumla nao wakapata mafunzo ambayo yatawawezesha kukabiliana na changamoto mbalimbali katika soko la ajira,”.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Angellah Kairuki akijadiliana jambo na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Dkt.Henry Mambo, katika moja ya hafla jijini Dar es Salaam hivi karibuni(Picha na Maktaba) .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Naomba kujua hiyo GPA ya 3.0 ni kwa wenye diploma tuu au na wale waliohitimu kidato cha sita na wenye total point 3 je nao wanaweza kujiunga shahada?

    ReplyDelete
  2. Jamani naomba kuuliza mtumishi wa serikali (PS) mwenye NABE II anaweza kujiendeleza na masomo ya uhazili ngazi ya Sertificate/Diploma?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...