NA HAJI NASSOR, PEMBA
TUME ya kurekebisha sheria Zanzibar, imeanza zoezi la kuwasilisha
miswada mitatu ya sheria ikiwemo ya uharibifu wa mazao, kwa
wadau mbali mbali kisiwani Pemba, baada ya kukusanya maoni ya
marekebisho ya sheria hizo, miezi iliopita.
Awali tume hiyo chini ya Mwenyekiti Jaji Mshibe Ali Bakari na Katibu
wake Asma Jidawi, walipita kwa wadau mbali mbali wakiwemo
masheha, wanasheria, wakulima na wananchi wengine kukusanya
maoni, ili kuzifanyia marekebisho sheria hizo kongwe.
Akiwasilisha mswada ya sheria ya Uharibifu wa mazao, mwanasheria
kutoka Tume hiyo Tajo Ameri alisema, kwa sasa baada ya maoni ya
wananchi, sheria inayokuja inatmbua uharibifu wa mazao mbali mbali,
badala ya ile ya zamani kuwa na mazao aina mbili pekee.
Alisema, jengine ambalo limo kwenye mswada huo ni kuingizwa kwa
mazao hata yanayotoka nje ya Zanzibar, ambapo mawali sheria hiyo ya
uharibifu wa mazao, ilitambua yale yanayozaliwa nchini pekee.
“Tulipita Unguja na Pemba kwa wadau mbali mbali, ili kukusanya maoni
juu ya sheria ya uharibifu wa mazao, na sasa tunayarejesha tena kwenu
ili kuona kama mliotueleza ndio”,alifafanua.
Kwa upande wake, mwanasheria wa Tume hiyo Miwta Khamis Haji,
alisema, suala la usajili wa nyaraka limekuwa ni jambo la lazima kwa
mali, kama vile mashamba na nyumba, ili kuondoa udanganyifu
unaoweza kujitokeza.
Mapema Katibu wa Tume hiyo ya Kurekebisha Sheria Zanzibar, Asma
Jidawi, alisema miongoni mwa kazi kubwa ya tume hiyo, ni kuzifanyia
marekebisho sheria au vifungu ambavyo vinaonekana kupitwa na
wakati.
Hata hivyo aliwataka wananchi na wadau wengine, kuendelea kutoa
maeoni yao kwa sheria mbali mbali, ambazo tume hiyo huzifanyia
marekebisho.
Baadhi ya masheha waliohudhuria mkutano huo, walisema elimu ya
usajili wa mali, nyaraka na ardhi inahitajika ili wananchi wapate elimu
ya kutekeleza sheria.
Shehe wa shehia ya Mgelema Omar Idd Zaina, alisema bado migogoro
ya ardhi hujitokeza kwa baadhi ya wamiliki kutokana na kukosa
uwelewa juu ya umuhimu wa kusajili ardhi zao.
Nae Sheha wa shehia ya Uweleni Abdalla Omar Mjawiri, aliipongeza
Tume hiyo, kutokana na kuwarejeshea maoni yao walioyakusanya
wakati zikifanyia marekebisho sheria za uharibifu wa mazao, usajili wa
nyaraka na sheria ya endelevu ya ardhi.
Tayari Tume ya Kurekebisha sheria Zanzibar imeshazifanyia
marekebisho sheria 17 ikiwemo sheria ya ushahidi, sheria ya wanyama,
vileo na sheria ya usafirishaji baharini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...