Na Alfred Mgweno - TEMESA Lindi

Mkandarasi aliyepewa kazi ya ujenzi wa maegesho ya kivuko katika maeneo ya Lindi na Kitunda tayari ameanza kazi hiyo na anatarajia kuikamilisha ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu. Akikagua maendeleo ya ujenzi huo, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu amemtaka Mkandarasi huyo kuhakikisha anamaliza kazi hiyo mapema iwezekanavyo hata kabla ya muda uliopangwa ili wananchi wa maeneo ya Lindi na Kitunda waanze kupata huduma ya kivuko.

Amesisitiza kuwa Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuondoa kero ya usafiri kwa wakazi wa maeneo hayo hivyo ujenzi wa maegesho hayo uende kwa kasi huku ukizingatia matakwa ya kiufundi na ubora wa hali ya juu.

Aidha Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Mkoa wa Lindi ambao ni msimamizi wa mradi huo, Mhandisi Margwe Boay alionyesha kuridhishwa na kasi ya ujenzi huo na kumtaka Mkandarasi kumaliza kazi hiyo mapema iwezekanavyo.

Mhandisi Boay, alimhakikishia Dk. Mgwatu kuwa wataisimamia kazi hiyo kwa kadri ya uwezo wao ili Mkandarasi akabidhi kazi ndani ya muda uliopangwa.

Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Hematec Investment Limited inayojenga maegesho hayo Mhandisi Emmanuel Lyimo, amesema mradi huo utakamilika kwa wakati na kuahidi kuwa kufikia mwisho wa mwezi Juni ujenzi wa maegesho upande wa Lindi utakuwa umefikia hatua nzuri na hatimae kuendelea na ujenzi upande wa Kitunda.
Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Lindi Mhandisi Margwe Boay (wa kwanza kulia) akielekeza jambo wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa maegesho ya kivuko kati ya Lindi na Kitunda unaoendelea mkoani hapo, wa pili kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dk. Mussa Mgwatu. Serikali inatarajia kupeleka kivuko eneo hilo mara baada ya ujenzi wa maegesho hayo kukamilika.
Mkurugenzi wa Ukodishaji Mitambo na Huduma za Vivuko wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle (wa nne kulia) akisisitiza jambo wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa maegesho ya kivuko kati ya Lindi na Kitunda unaoendelea mkoani Lindi, kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dk. Mussa Mgwatu.
Mkandarasi wa kampuni inayojenga maegesho ya kivuko kati ya Lindi na Kitunda Mhandisi Emmanuel Lyimo (wa kwanza kulia) akimuelekeza jambo Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dk. Mussa Mgwatu wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa maegesho unaoendelea mkoani Lindi. Serikali inatarajia kupeleka kivuko mara baada ya ujenzi wa maegesho hayo kukamilika.
Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Lindi Mhandisi Margwe Boay (wa pili kulia) akielekeza jambo wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa maegesho ya kivuko kati ya Lindi na Kitunda unaoendelea mkoani hapo, wa pili kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dk. Mussa Mgwatu. PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO (TEMESA)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...