THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

UKAGUZI MABASI WA KITUO KIKUU CHA MABASI UBUNGO

Mkaguzi wa Polisi katika Kituo cha cha Mabasi Ubungo, Inspekta Ibrahim Samwix akikagua moja ya basi katika kituo hicho kikuu cha mabasi ya mikoani na nje ya nchi leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni utaratibu wa ukaguzi kabla ya mabasi hayo hajaanza safari.
Mkaguzi wa Polisi katika Kituo cha cha Mabasi Ubungo, Inspekta Ibrahim Samwix katika uvungu wa basi akikagua basi katika kikuu cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani.
Askari wa Kikosi cha usalama barabarani kituo cha Ubungo, Nuru Mvungi akikagua mikanda katika basi la Kampuni ya Mlola inayofanya safari zake Dar es Salaam na Tanga leo jijini Dar es Salaam.
Askari wa Kikosi cha usalama barabarani kituo cha Ubungo, akionesha basi la Cheeter linalofanya safari zake Dar es Salaam na Dodoma likiwa limetolewa namba za usajili kutoka na ubovu na basi hilo linatakiwa kufanya safari baada kufanyiwa marekebisho leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya mabasi yakiwa katika kituo kikuu cha Ubungo leo jijini Dar es Salaam.


Hoja moja imeshachangiwa mpaka sasa.

  1. Usalama kwanza....big up sana Inspector Samwix kwa kuongoza kwa vitendo. Kwa nini zoezi la hivi lisifanyike nchi nzima ili kupunguza kabisa wimbi la ajari?!!...tafakari