Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Upelelezi dhidi ya kesi ya kumshambulia askari polisi inayomkabili aliyekuwa Naibu Waziri wa fedha na mbunge wa Mkuranga, Adam Kigoma Malima umekamilika.

Mwendesha Mashtaka, Wakili wa Serikali Esta Martin amemueleza Hakimu Mkazi, Godfrey Mwambapa wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa kesi hiyo leo ilikuja kwa kutajwa."Mheshimiwa, kesi hii Leo imekuja kwa kutajwa lakini upelelezi umekamilika, tu naomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuja kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali (PH), amedai Martin.

Hakimu Mwambapa ameiahirisha kesi hiyo kwa niaba ya Hakimu Mkazi Respecious Mwijage ambaye ndio amepangwa kusikiliza kesi hiyo kwa kuwa anaudhuru.

" Hakimu aliyepangwa kusikiliza kesi hii anaudhuru, naiahirisha hadi Julai 10 itakapokuja kwa ajili ya kusomewa PH mbele ya Hakimu husika", amesema Hakimu Mwambapa

Malima anashtakiwa pamoja na dereva wake Ramadhani Mohamed Kigwande anayekabiliwa na tuhuma za kujeruhi.Katika hati ya mashtaka ilidaiwa kuwa, Mei 15 mwaka huu huko Masaki katika wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam mshtakiwa Malima alimzuia afisa wa polisi mwenye namba H.7818 PC Abdul kufanya kazi yake ya kumkamata dereva wake Kigwande aliyekuwa amefanya kosa la kumjeruhi Joseph Mwita ambaye ni afisa operation wa Priscane Business Enterprises.

Ilidaiwa kuwa, siku na mahali hapo, mshtakiwa Kigwande kwa nia ya kukataa kukamatwa, alimjeruhi afisa operation hiyo(Joseph Mwita) ambaye alikuwa anakamatwa kwa kosa la kupaki gari vibaya na kumsababishia Mwita Majeraha Mwilini.

Watuhumiwa wote wako nje kwa dhamana na upelelezi bado haujakamilika.

Aidha, Wakili wa utetezi Peter Kibatala ameshindwa kuwasilisha pingamizi la awali juu ya mapungufu ya kisheria yaliyopo kwenye shtaka la shambulio linalomkabili Malima Peke yake kwa kuwa Hakimu husika anaudhuru.

Mapema mwzi huu, Kibatala aliitaarifu Mahakama kuwa leo angewasilisha pingamizi kuwa shtaka linalomkabili Malima, maelezo ya kosa na tuhuma hazifanani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...