· Waunga mkono kampeini ya kitaifa ya usafi wa mazingira

Mashirika ya kimataifa yanayounga mkono juhudi za serikali kuwezesha upatikanaji wa maji safi na salama leo kwa pamoja yameunga mkono kampeni ya kitaifa ya usafi ijulikanayo kama Niko Tayari inayoendeshwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Mashirika hayo ni UNICEF (Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto), Benki ya Dunia, Shirika la misaada la Uingereza (DFID), Shirika la Miradi la Ujerumani (GIZ) na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA). Wawakilishi wa mashirika hayo walikutana kwenye ukumbi wa mikutano, Ubungo Maji, jijini Dar es salaam leo.

Mashirika hayo ya maendeleo yamekubali kuunga mkono kampeini hiyo ilizinduliwa mwezi uliopita mjini Dodoma ikiwa na lengo la kuhamisha usafi wa mazingira kwa kila Mtanzania hasa kuwa na choo katika kila familia na kujenga utamaduni wa kunawa mikono baada ya matumizi yake. Kwa kufanya hivyo kutasaidia kupunguza vifo hivyo kusaidia ukuaji wa uchumi nchini.

Akiongea na waandishi wa habari, Mratibu wa kampeini ya Nipo Tayari Anyitike Mwakitalima kutoka Wizara ya Afya alisema ili kuwa na huduma bora ya maji, usafi wa mazingira ni muhimu kuzingatiwa. ‘Kwa kujitokeza wadau wetu wa Maendeleo na kuunga mkono kampeini yetu ni kitu cha kupogezwa sana na pia niishara kwamba malengo yetu ya kuwa na mazingira salama yatafanikwa’, alisema Mwakitalima. 

Zaidi ya mashirika 10 ya maendeleo ya kimataifa yamejitokeza kuunga mkono kampeini hiyo inayojumuisha mikoa yote Tanzania Bara.

Kampeini hiyo ya usafi wa mazingira na matumizi bora ya choo (NikoTayari) inatarajiwa kuwa chachu ya upatikanaji wa maji safi na salama na kuboresha afya za Watanzania wote, mijini na vijijini. 



Afisa Afya Mkoa wa Pwani Emmanuel Mwandepa akitoa ishara ya Nipo Tayari kuunga mkono kampeni ya taifa ya usafi wa mazingira wakati wa mkutano wa wadau wa maji uliofanyika jana jijini Dar es Salaam. Kampeni hiyo iko chini ya Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii ikiwa na lengo la kuhamasisha usafi wa mazingira na matumizi ya choo bora.


Mwakilishi wa TAMISEMI, Idara ya Afya, Mwajina Lipina akitoa ishara ya Nipo Tayari kuunga mkono kampeini ya Taifa ya usafi wa mazingira wakati wa mkutano wa wadau wa maji uliofanyika jana jijini Dar es Salaam. Kampeni hiyo iko chini ya Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii ikiwa na lengo la kuhamasisha usafi wa mazingira na matumizi ya choo bora.

Mratibu wa huduma ya maji na usafi wa mazingira shule kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Technolojia Theresia Kuiwipe akitoa ishara ya Nipo Tayari kuunga mkono kampeni ya Taifa ya usafi wa mazingira wakati wa mkutano wa wadau wa maji uliofanyika jana jijini Dar es Salaam. Kampeni hiyo iko chini ya Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii ikiwa na lengo la kuhamasisha usafi wa mazingira na matumizi ya choo bora. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...