Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
Wadau
na wachumi mbalimbali wametoa maoni tofauti kuhusu bajeti ya serikali
ya mwaka 2017/2018 iliyowasilishwa jana Bungeni na Waziri wa fedha na
Mipango, Dk. Philip Mpango na kusema kuwa ni mapema mno kuisherehekea.
Wakizungumza
katika mkutano wa kujadili bajeti hiyo ulioandaliwa na kampuni ya
ukaguzi ya Ernst and Young (EY),wamesema, ni vema kusubiri mabadiliko ya
sheria ya fedha ili kuja kuona mpango wa utekelezaji wake.
Mkurugenzi
wa Utawala na Kodi wa Kampuni ya Ukaguzi ya EY (Ernest & Young),
Laurian Justinian akizungumza wakati wa Mkutano wa Wadau na
Wachumi mbali mbali wa kujadili Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha
2017/18, ulioandaliwa na Kampuni ya Ukaguzi ya EY (Ernest & Young),
katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar es
salaam Juni 9, 2017.
Wameongeza
kuwa, uzoefu unaonyesha kuwa, mara nyingi bajeti inakuwa na mambo
mazuri lakini utekelezaji wake unakuwa ni tofauti kwani hata ile
iliyopita utekelezaji wake haukuridhisha.
Wamesema
kuwa, ni vizuri wananchi wakaacha kusherehekea badala yake kuona
utekelezaji na kama ikibidi waje washerehekee mwezi Juni mwakani.
Akitoa
maoni yake katika majadiliano hayo Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe
na Mshauri wa Uchumi, Profesa Honest Ngowi amesema bajeti ya mwaka jana
haikutimia kabisa, malengo yalikuwa kukusanya Tirioni 29.5 lakini
ilipatikana Tirioni 20.1 ambayo ni sawa na asilimia 70.1 na bajeti ya
mwaka huu ni Tirioni 31.6 ongezeko la tirioni 11. je nini kitafanyika
kupata fedha hizo za mwaka huu.
Amesema
kuwa kuna masuala mengi ambayo ni lazima yaelezewe sheria ya fedha kwa
jinsi itakavyokuwa inatekelezwa ikiwa ni pamoja na kupunguza misamaha
isiyokuwa ya lazima.
Amesema
bajeti hii inaleta neema kwa wakulima ambao walikuwa wanalipa tozo kwa
ukomo wa asilimia tano lakini sasa watakuwa wakilipia ukomo wa asilimia
tatu tu.
Aidha
ameongeza pia kuondolewa kwa kodi ya leseni Ya magari kutawapunguzia
wananchi mzigo mkubwa, hasa wale ambao magari yao hayakuwa yakitumia
klwa muda mrefu lakini bado yalikuwa yanahesabiwa kodo kama kawaida.
Ameongeza
kuwa, uchumi wa Tanzania na Africa Mashariki kwa ujumla unaenda kwenye
viwanda, na kuna mambo mengi ya kikodi yamejitokeza ya kulinda viwanda
vya ndani kwa maana hiyo kuongezeka kwa kodi kwenye vitu vitakavyokuwa
vinaingia ndani yan chi hizo kutakuwa kunalinda soko la ndani.
“Changamoto
kubwa itakuwa namna ya kupata fedha zote hizo Tilioni (31.6) hatujajua
ni nini cha tofauti kimefanywa tofauti na miaka mingine kusudi kuweza
kupata fedha hizo ambazo kwa mwaka jana tulishindwa kupata 29.5
tukaishia kugonga kwenye Trn 20.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe na Mshauru wa Maswala ya Fedha na
Uchumi, Prof. Honest Ngowi akizungumza wakati wa Mkutano wa Wadau na
Wachumi mbali mbali wa kujadili Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha
2017/18, ulioandaliwa na Kampuni ya Ukaguzi ya EY (Ernest & Young),
katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar es
salaam Juni 9, 2017.
Ameongeza
kuwa ili kuweza kujaribu kufikia lengo hilo TRA wanatakiwa kukusanya
kodi kistaarbu bila ya kutumia nguvu na mabavu, Mkurugenzi wa kodi wa EY
Laurian Justinian amesema bajeti inamuelekeo mzuri, inaaanza kuonyesha
picha ya kuingia kwenye viwanda but kunamasuala yanatakiwa kuwa na
wiano.
Muanzilishi
na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Pangani group Heri Bomani amesema
Serikali imekuwa ikiwekeza zaidi kwenye miundombinu na sasa inahama
kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma.
Muanzilishi
na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Pangani Group, Heri Bomani
akizungumza wakati wa Mkutano wa Wadau na Wachumi mbali mbali wa
kujadili Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/18, ulioandaliwa na
Kampuni ya Ukaguzi ya EY (Ernest & Young), katika Ukumbi wa Mikutano
wa Hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar es salaam Juni 9, 2017. Wengine
pichani kutoka kulia ni Mhadhili wa Chuo Kikuu cha Mzumbe na Mshauru wa
Maswala ya Fedha na Uchumi, Prof. Honest Ngowi, Mkufunzi, Mtafiti na
Mshauri kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe, Dkt. Faisal Issa pamoja na
Mkurugenzi wa Utawala na Kodi wa Kampuni ya Ukaguzi ya EY (Ernest &
Young), Laurian Justinian.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...