Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ameuagiza Uongozi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kupeleka wahandisi wa kutosha katika ujenzi wa Gati ya Mtwara ili kupata uzoefu katika kazi za ujenzi.

Akizungumza mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Bandari hiyo Waziri Prof. Mbarawa amesema ushiriki wa wahandisi hao utasaidia kuwajengea uzoefu mkubwa na hivyo kuokoa fedha nyingi ambazo zitatumika kwa kuwatumia wahandisi wa kigeni.

“Mradi huu unagharimu fedha nyingi hivyo ni muhimu wahandisi wa TPA wakaja kujifunza kwa vitendo ili mradi utakapokamilika wahandisi wetu watumike kufanya ukarabati na matengenezo badala ya kusubiri kuwaleta tena wahandisi kutoka nje”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Amesisitiza uongozi wa TPA kutafuta wahandisi waliomaliza vyuo nchini ili waweze kujifunza kwa vitendo kupitia mradi huo kama sehemu ya mafunzo kwa vitendo ili kupata uzoefu.

Kwa upande wake, Meneja wa bandari ya Mtwara, Eng. Juma Kijavara, amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa tayari utekelezaji wa agizo la kutafuta wahandisi hao umeshaanza na hatua inayofata ni kuwasili kwa wahandisi hao eneo la madi.

Upanuzi wa bandari ya Mtwara utahusisha awamu nne na awamu ya kwanza ambayo itagharimu kiasi cha Tsh. bilioni 137 na inatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 22, kukamilika kwa gati hiyo kutaiwezesha bandari hiyo kuhudumia meli ya ukubwa wa mita 300 na kukuza uchumi wa mkoa huo kupitia usafirishaji wa gesi, saruji, korosho pamoja na makaa mawe.
Meneja wa Bandari ya Mtwara, Eng. Juma Kijavara (kulia), akimuonyesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, eneo ambalo ujenzi wa gati ya pili ya bandari hiyo utakapoanza kujengwa wakati Waziri huyo alipokagua vifaa vya Mkandarasi vilivyowasili katika eneo la mradi hivi karibuni.
Baadhi ya Vifaa ambavyo vitatumika katika ujenzi wa gati ya pili ya bandari ya Mtwara vikiwa vimeshawekwa site tayari kwa kuanza ujenzi. Ujenzi huo unakadiriwa kukamilika ndani y amiezi 22.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (mwenye suti ya Blue), akiangalia vifaa vitakavyotumiwa na Kampuni ya M/S China Railways Construction Engineering Group (CRCEG) na M/S China Railways Major Bridge Engineering Group Co. ltd (CRMBEG) katika ujenzi wa gati ya pili ya bandari ya Mtwara, mkoani humo hivi karibuni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...