Wahasibu zaidi ya 130 kutoka halmashauri za wilaya za mikoa ya Kanda ya Ziwa na Kati wamepatiwa mafunzo ya Mfumo wa Kielekroniki kuhusu Usimamizi wa fedha ngazi za msingi zikiwemo zahanati,vituo vya afya,hospitali na shule za msingi na sekondari.

Mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa mfumo wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma ‘Facility Financial Accounting and Reporting System – FFARS) kupitia mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma ‘ Public Sector Systems Strengthening – PS3’ unaotarajiwa kuanza kutumika Julai 1,2017 katika halmashauri mbalimbali nchini.

Wahasibu hao wanashiriki katika mafunzo yanayofanyika katika ukumbi wa Vigimark Hotel Mjini Shinyanga ambayo yamekutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wawakilishi kutoka PS3,TAMISEMI,Wizara ya afya,wizara ya elimu.

Mwezeshaji wa Mafunzo hayo, Elizeus Rwezaula ambaye ni Mshauri wa Masuala ya Usimamizi wa Fedha za Umma kutoka Mradi wa HPSS Dodoma,alisema mfumo wa kutumia njia za kielektroniki (kompyuta) katika kuingiza taarifa za kifedha za vituo vya kutolea huduma unasaidia kurahisisha kazi.

“Katika Afrika Mashariki,Tanzania ndiyo nchi pekee itakayoanza kutumia mfumo huu wa kisasa wa kielektroniki katika uingizaji taarifa za fedha katika ngazi za msingi za kutolea huduma,na umetengezwa na vijana wa hapa nchini ili kuhakikisha kuwa mfumo wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma (FFARS) unafanikiwa”,alieleza Rwezaula.

Afisa Msimamizi wa Fedha Mwandamizi TAMISEMI, Elisa Rwamiago akizungumza wakati wa mafunzo kuhusu mfumo huo kupitia mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma ‘ Public Sector Systems Strengthening – PS3’ unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID)

Afisa Msimamizi wa Fedha Mwandamizi TAMISEMI, Elisa Rwamiago akielezea kuhusu mfumo wa kielektroniki katika ujazaji taarifa za fedha katika vituo vya kutolea huduma.

Afisa Msimamizi wa Fedha Mwandamizi TAMISEMI, Elisa Rwamiago akizungumza ukumbini

Mwezeshaji wa Mafunzo ya FFARS ,Elizeus Rwezaula ambaye ni Mshauri wa Masuala ya Usimamizi wa Fedha za Umma kutoka Mradi wa HPSS Dodoma,akitoa mada kuhusu njia/mfumo wa kielektroki katika ujazaji taarifa za fedha katika vituo vya kutolea huduma 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...