Na Tiganya Vincent.

WAISLAMU Mkoani Tabora wametakiwa kuunga mkono juhudi zilizoanzishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli za kupambana kikundi la watu wachache ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakinufaika na rasilimali ya nchi hii na kuwaacha watu wengi wakiwa maskini licha ya utajiri waliojariwa na Mungu.

Kauli hiyo imetolewa jana mjini Tabora na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ibrahim Mavumbi wakati wa futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa huo Bw. Aggrey Mwanri.

Alisema kuwa Rais Magufuli haipaswi kuachiwa pekee vita aliyoanzisha , bali anatakiwa kuungwa mkono na watu wote wenye mapenzi mema na nchi hii kwani kiongozi huyo amesaidia kuwafumbua macho na kuona kuwa wameibiwa sana na walikuwa wakiendelea kuibiwa na kikundi cha watu wachache kwa maslahi yao binafsi na sio ya watu wengi.

Sheikh Mavumbi aliongeza kuwa Rais Magufuli ameonyesha mapenzi makubwa kwa nchi yake na wananchi wake na kukwerwa na umaskini wa wananchi wake uliosababishwa na tamaa ya watu wachache waliokuwa wakinufaika wakati nchi ikibaki na mashimo ambayo wakati mwingine yanaweza kusababisha vifo kwa watu kutumbukia ndani yake.

Alisisitiza kuwa sio vizuri kupuuza juhudi kubwa anaozifanya Rais Magufuli kwa kushirikiana na viongozi wenzake za kusimamia rasilimali za nchi na kutetea haki za wanyonge ambao walikuwa wakidhulumiwa na watu wachache  kwa maslahi yao binafisi

Sheikh Mavumbi aliongeza kuwa Rais Magufuli anataka kutupeleka ambapo kila raia wa nchini hii atakunufaika na utajiri wa nchi hii ambao wamejariwa na Mungu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...