Frank Mvungi-Maelezo.

Takriban wakazi 234,398 wa  Chalinze watanufaika na  mradi wa upanuzi wa mtambo na ujenzi wa mfumo wa kusafirisha na kusambaza maji safi pamoja na matenki ya kuhifadhi unaolenga kuondoa changamoto ya upatikanaji wake katika Jimbo hilo.

Akizungumza  kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa hafla ya kukagua maendeleo ya mradi  huo, Waziri wa Maji na Umwagiliaji,  Mhandisi Gerson Lwenge amesema kuwa Serikali inaridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi huo na kumtaka mkandarasi kuongeza kasi katika kutekeleza mradi huo.

“Dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa wananchi wanapata maji safi na salama ndio maana tumeweka wataalamu wetu hapa kumsimamia mkandarasi ili afanye kazi  kwa ubora na kwa kasi kama ambavyo Waziri Mkuu aliagiza alipotembelea mradi huu mwezi Machi mwaka huu”, alisisitiza Lwenge.

Akifafanua, Mhandisi Lwenge amesema kuwa hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa  mradi huo awamu ya tatu ni ulazaji wa mabomba ya kusafirisha na ya kusambaza maji, ujenzi wa matanki 19, na ujenzi wa  mtambo wa kusafishia maji ambao unaendelea. 

Kazi nyingine zinazoendelea katika kutekeleza mradi huo ni ujenzi wa vituo 351 vya kuchotea maji ambapo vituo 27 vimekamilika,vituo 226 vipo katika hatua mbalimbali na vituo 98 havijaanza kujengwa.

Akizungumzia hatua zinazochukuliwa na mkandarasi wa mradi huo, Mhandisi Lwenge amesema kuwa ni kuongezeka kwa upatikanaji wa vifaa kwa wakati katika eneo la mradi, kuongeza wafanyakazi na maeneo ya kazi na kuteua mwakilishi wa kampuni anayeweza kutoa maamuzi kwa niaba ya kampuni inayotekeleza mradi.

Aidha, Waziri Lwenge amesema kuwa Serikali itatoa ufumbuzi wa changamoto ya wananchi wa Jimbo hilo kulipia malipo ya huduma  (service charge) hata pale wanapokuwa hawajapata huduma hiyo ili kuwe na utaratibu mzuri unaowezesha wananchi kulipia huduma pale wanapotumia tu na si vinginevyo.
 Moja ya tenki la maji linalojengwa katika chanzo cha maji cha mto Ruvu ikiwa ni sehemu ya mradi huo.
 Mbunge wa Jimbo la ChalinzeChalinze, Mhe. Ridhiwan Kikwete akimshukuru Waziri wa Maji na Umwagiliaji  Mhandisi Gerson Lwenge kwa hatua nzuri iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi huo.

Mafundi wakiendelea na maandalizi ya ujenzi wa matenki yakuhifadhi maji katika chanzo cha maji Ruvu. (Picha zote na Frank Mvungi-Maelezo).

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...