Wananchi wa kata ya Chilonwa, wilaya Chamwino mkoani Dodoma wameiomba Serikali kuchukua hatua za haraka kujenga daraja la Chilonwa lililopo katika kata hiyo ili kutatua kero ya usafiri kwa wananchi hao na maeneo jirani hususan katika kipindi cha masika. 

Wakieleza kero yao kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, wananchi hao wamesema wanaamini kuwa ujio wa Naibu Waziri huyo katika kata yao kutaleta ufumbuzi wa kero hiyo.

“Tunaamini sasa tutapata mwarobaini wa daraja hili kwani tatizo hili ni la muda mrefu, siku hadi siku daraja linakuwa fupi kutokana na kufukiwa na mchanga na hivyo hupelekea maji kujaa darajani hapa kipindi cha masika na watu kushindwa kuvuka”, amesema mmoja wa wananchi hao.

Aidha, wananchi hao wamemwomba Naibu Waziri huyo kurekebisha daraja hilo kwa kulijenga juu zaidi ili kupitisha maji na kupitika katika vipindi vyote vya mwaka kutokana na kwamba lililopo sasa lipo chini zaidi mara baada ya kufukiwa na mchanga.

Wananchi hao wameeleza masikitiko yao kwa Naibu Waziri huyo hususan katika kipindi cha masika ambapo wamesema hutumia kiasi cha shilingi elfu kumi kuvushwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine na wengine hupoteza maisha wakiwa wanavuka.
Muonekano wa Daraja la Chilonwa lililopo kata ya Chilonwa, wilayani Chamwino mkoani Dodoma. Daraja hilo ni kiungo kati ya mkoa wa Dodoma, Manyara na Arusha. 
Sehemu ya daraja la Chilonwa iliyoathirika kutokana na shughuli za kibinaadamu kama vile kilimo na hivyo kupelekea kwa daraja hilo kufukiwa na mchanga na kuwa fupi. 

Mbunge wa jimbo la Chilonwa, Mhe. Joel Makanyaga, akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani (kushoto kwa Mbunge), alipofika jimboni hapo kukagua daraja la Chilonwa, wilayani Chamwino mkoani Dodoma leo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...