THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

WANAOLIMA KWENYE MAENEO OEVU WAONDOKE- RC MASENZA


Na matukiodaimaBlog

SERIKALI Imewataka wananchi wanaolima kilimo kwenye maeneo oevu maarufu kama vinyungu kutafuta shughuli nyingine ya kufanya nje ya kilimo hicho kulinda mto Ruaha mkuu kukauka.

Akitoa salam za mkoa wa Iringa wakati wa sherehe ya tuzo ya TANAPA ya uhifadhi mazingira na kilele cha siku ya mazingira Duniani leo maadhimisho yaliyofanyika kwa kijiji cha Madabaga wilaya ya Mbarali mkoa wa Mbeya Jana mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza alisema iwapo ulimaji wa vinyungu utafumbiwa macho mto Ruaha mkuu utaendelea kukauka.

Alisema kuwa chanzo kikubwa cha uharibifu wa ikolojia ya mto Ruaha mkuu pamoja na hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

Kwani alisema uhifadhi wa hifadhi ya Ruaha ni pamoja na uhifadhi wa mto Ruaha mkuu hivyo mikoa ya Iringa,Njombe na Mbeya wana wajibu wa kulinda mto Ruaha mkuu na kuchukua hatua kwa wote wanaolima kwenye vyanzo vya maji.

Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza kulia na mkuu wa wilaya ya Kilolo   Asia Abdalah wakimpongeza mwakilishi wa kikundi cha familia ya Festo Mhanga wa Kilolo kwa kushinda tuzo ya Mazingira ya Tanapa na kuzawadiwa shilingi milioni jana wakati wa kilele cha siku ya Mazingira na utoaji wa Tuzo za TANAPA kwa wananchi wa mikoa ya Iringa , Njombe na Mbeya

Mgeni rasmi katika kilele cha siku ya mazingira duniani jana Amos Makala mkuu wa mkoa wa Mbeya akiteta jambo na mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza na meneja ujirani mwema wa Tanapa Ahmed Mbugi kushoto .

Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akitoa salam siku ya Mazingira Duniani mkoani Mbeya .

Kikundi cha skauti cha elimisha jamii wilaya ya Mufindi wakikabidhiwa hundi ya shilingi milioni 1 toka Tanapa .