THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

WAONGOZA UTALII WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KATIKA KUWAPENDEKEZA WATAKOINGIA KATIKA KINYANG'ANYIRO CHA KUMPATA MUONGOZAJI BORA WA MWAKA 2017

Na.Vero Ignatus Kilimanjaro.

 Wito umetolewa kwa waongoza watalii nchini kutoa ushirikiano ,kuwapendekeza watakaoingia katika kinyang'anyiro cha kumtafuta mshindi wa Tuzo ambayo imeandaliwa kwaajili ya kumpata Balozi atakaewawakilisha waongoza utalii nchini Tanzania,Afrika ya Mashariki na Kati .

Akizungumza na blog hii Muasisi na mwenyekiti wa Tuzo hiyo Sadock Mugetta amesema kuwa tuzo  inafahamika kama  TANZANIA TOUR GUIDE AWARDS   ambapo mwaka jana ilikuwa imegawanyika   katika vipengele vya kumtafuta muongoza watalii bora wa Mlima,Safari pamoja na Wapagazi,ila mwaka huu wameongeza vipengele viwili ambavyo ni Muongoza utalii wa Utamaduni pamoja na Mpishi bora.

Sadock amesema kuwa wameamua kuwepo kwa Tuzo hiyo kutokana hali halisi iliyopo ya ugumu wa kazi wanayoifanya waongoza watalii (Mabalozi) ili mshindi atakayepatikana atawawakilisha katika mambo yao ambayo wanataka Serikali iyafahamu,pamoja na wageni mbalimbali waitambue Tanzania pamoja na vivutio vya Utalii vilivyopo.

 Ameongeza kuwa tangia kuanzishwa kwa huduma ya  utalii hapa nchini waongoza Watalii  hawajawahi kupewa kipaumbele, hivyo ni vyema Serikali ikatambua kuwa muongozaji watalii huwa  anatumumia 99% ya muda wao  kukaa na mgeni awapo nchini na anapewa taarifa zote sahihi na muhimu  hadi anaondoka nchini. 
Wa kwanza kushoto ni Muasisi wa Tanzania Tour Guide Awards Sadock Mugetta, aliyepo kushot kwake ni Katibu wa Freelance Guides Society of Tanzania(FGST )anayefuata ni mjumbe wa  wakiwa katika maonyesho ya (3)Utalii ya Kilifair  katika uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro.