THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

WASHINDI WA LIGI YA CHUO CHA TEKU MBEYA WAPEWA ZAWADI ZAO

Katika hekaheka za  kusherehekea Sikukuu ya Eid El Fitr Uongozi wa Chuo Kikuu Teofilo Kisanji (TEKU) cha Jijini Mbeya kwa kushirikiana na Serikali ya Wanafunzi TEKUSO na mmoja wa wadau wakubwa wa Vijana,Amani Kajuna wamefanya bonanza kubwa la michezo kwa kuzishirikisha Timu mbalimbali kutoka ndani ya Chuo na nje ya Chuo ambapo Timu kutoka Mbozi, Uyole, Madereva Bajaji, Madereva Bodaboda zilishiriki kikamilifu kwenye mpira wa miguu, kikapu, pete na mpira wa wavu.

Katika mashindano hayo washindi walikabidhiwa zawadi zao na Makamu Mkuu wa Chuo Dkt. Daniel Mosses kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mjini Mhe. William Ntinika, aliyefungua bonanza hilo na baadaye kuhutubia umati uliokuwepo Chuoni hapo.

Awali, Makamu Mkuu wa Chuo TEKU-Taaluma Dkt. Daniel Gwakisa alisema "Chuo chetu kimekuwa kikijitambulisha kwa Taaluma yake bora na pia kupitia Michezo, kwani tunaamini vipaji vya Vijana wetu vinapaswa kuendelezwa ili vikue zaidi", alisema na kuongeza kuwa Mhadhiri wa Wanafunzi TEKU Mkufunzi Bi. Stella Seif amesema TEKU wanawalea Vijana (Wanafunzi)  kwa misingi bora kwa kutambua mahusiano ya kada za Cheti, Diploma, Shahada na kada zingine kama za Uzamili.

Katka ufafanuzi wake alipokuwa akizungumza na Mwandishi wetu ,Rais wa Serikali ya Wanafunzi (TEKUSO) Mhe. Byula Mahona amewaalika wazazi na wanafunzi waliomaliza Elimu za Sekondari na Vyuo kuja kujiunga na Chuo cha TEKU,kwani ni Chuo pekee Jijini Mbeya kinachojali na kukuza vipaji vya wanafunzi huku Taaluma itolewayo ni bora.

Alisema moja ya mafanikio ya kukuza vipaji vya wanafunzi ni Chuo kumtoa Miss Mbeya 2016 Eunice John Robert ambaye alishiriki Shindano la Miss Tanzania 2016 na kufanikiwa kutwaa taji la Miss Tanzania Personality 2016, aidha kuna vijana wengine wenye vipaji kama Mzee wa Madodoso, Mpoli Daudi (Wachekeshaji), Goliath, D-nax, G-mafic, Ekka da Music, Peff Mc, Ndaki Black (Wanamuziki) nao wakiwa ni miongoni mwa Vipaji kutokea Chuoni hapo.
Matokeo ya Michezo ya Bonanza yalikuwa kama ifuatavyo: NETBALL:- Teku Queens goli 20 Vs Uyole Queens goli 11 (Mshindi amepata Tshs 50,000/=), BASKETBALL:- Worriers Vikapu 54 Vs Teku Vikapu 50 (Mshindi amepata Tshs 50,000/=), VOLLEYBALL;- Vijana Jiji set 2 Vs Teku set 3 (Mshindi amepata Tshs 50,000/=), Mpira wa miguu kulikua na Timu nne, Bodaboda Fc 2-1 Bajaji Fc,  Unity Fc toka Mbozi 2-1 Home Boys toka Chunya hivyo Fainali ilikuwa kati ya washindi Bodaboda Fc Vs Unity Fc (Dakika 90,Unity Fc 1-1 Bodaboda Fc, mikwaju ya penati Bodaboda Fc 4-5 Unity Fc (Mshindi wa kwanza Tshs 100,000/= wa pili Tshs 50,000/= zilitolewa) 

Mara baada ya mchezo huo kukamilika ndipo mchezo wa Fainali ya Ligi ya Chuo ulichezwa kati ya Timu ya BAED mwaka wa kwanza Vs Timu ya BEDMATHS mwaka wa pili, Matokeo;- BAED 3-2 BEDMATHS (Mshindi wa kwanza amepata Tshs 400,000/= na wa pili Tshs 100,000/=)