Na Frank Mvungi-Maelezo

Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imetoa mafunzo kwa wasindikaji wadogo wa vyakula 1287 tangu mwaka 2013 ili waweze kusindika vyaklula vyenye ubora kwa mujibu wa sheria na kanuni za uzalishaji na kuhimili ushindani wa soko.

Akifungua mafunzo ya wasindikaji wadogo wapatao 60 wa vyakula yaliyoratibiwa na Mamlaka hiyo leo jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Bw. Hiiti Sillo, Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula Bw. Raymond Wigenge, amesema dhamira ya Serikali ni kuwawezesha wajasiriamali wadogo hapa nchini.

“Kukua kwa viwanda hivi kutakuwa na mchango mkubwa katika kuongeza ajira na kipato katika ngazi ya kaya, kukuza kilimo cha mazao ya chakula kutokana na kuwepo kwa soko la mazao ya vyakula”. Alisisitiza Wigenge.

Akifafanua Wigenge amesema Serikali inatambua kuwa viwanda vidogo vina nafasi kubwa ya kuchangia pato la Taifa hasa katika kipindi hiki ambacho Serikali inasisitiza ujenzi wa uchumi wa Viwanda.

Alieleza kuwa Mamlaka hiyo imeingia mkataba wa maridhiano (MOU) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ambapo mchango wa taasisi hizo mbili utatambuliwa katika tasnia ya ujasiriamali wa bidhaa zinazodhibitiwa na Mamlaka.

Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw. Raymond Wigenge akifungua mafunzo ya wasindikaji wadogo wa vyakula (hawapo pichani) ambayo yaliatibiwa na Mamlaka hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Ukaguzi na Ufuatiliaji wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw. Justin Makisi akitoa ufafanuzi kuhusu umuhimu wa mafunzo kwa wasindikaji wadogo wa vyakula.
Mwenyekiti wa Chama cha Kuweka na Kukopa Wajasiriamali Wadogo Tanzania (TASWE) na muwakilishi wa wanawake wajasiriamali Bi. Anna Matinde akipongeza juhudi za Serikali katika kuwawezesha wajasiriamali wadogo hapa nchini. Kulia ni Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula wa Mamlaka hiyo Bw. Raymond Wigenge na kushoto ni Afisa Udhibiti Ubora Bi. Prisca Kuela
Baadhi ya wajasiriamali wakifuatilia mafunzo yaliyoratibiwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa Nchini (TFDA) kwa wasindikaji wadogo wa vyakula .
Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw. Raymond Wigenge akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Bw. Hiiti Sillo wakati wa mafunzo ya wasindikaji wadogo wa vyakula.(Picha zote na Frank Mvungi-Maelezo)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...