NA K-VIS BLOG/Khalfan Said 

Katika hotuba yake aliyotoa Kati wa ufunguzi rasmi wa semina hiyo, Bw. Mayingu alisema, PSPF inatarajia kulipa wastaafu kiasi cha shilingi Trilioni 1.3 kwa mwaka huu tu wa 2017/18."Kwa mwaka 2017/18 pekee, Mfuko unatarajia kuwalipa wastaafu 9,552 jumla ya mafao yanayofikia shilinginTrilioni 1.3.

Kisai hiki cha Mafao ni kikubwa, hivyo kupitia semina hii Wastaafu watarajiwa wa PSPF wamejifunza namna ya kupanga maisha yao baada ya kustaafu ikiwa ni pamoja na fursa za uwekezaji wa mafao yao ili mafao haya yaweze kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya uchumi na kuongeza fursa za ajira." Alisema Bw. Mayingu katika hotuba yake. 

Miongozi mwa mambo waliojifunza wastaafu hao wanaokadiriwa kufika 450, ni pamoja na uanzoshwaji wa viwanda vidogo vidogo, namna bora ya utunzaji fedha kwenye taasisi za fedha, (mabenki), lakini pia mbinu mbalimbali za ujasiriamali. 

Kuhusu mafunzo yaliyotolewa na SIDO, Bw. Mayingu alisema Mfuko ulikutana na Shirika la Kuhudumia Viwanda vidogo vidogo (SIDO) na kujadiliana namna ambavyo taasisi hizi mbili zinaweza kushirikiana na kuwafanya wastaafu wa PSPF wapate ujuzi wa kuwekeza na kuweza kutengeneza ajira kwa vijana. 

"Lengo likiwa SIDO iwajengee uwezo kitaalamu na kuwapatia vifaa ili wastaafu wa PSPF waweze kuanzisha viwanda vidogo vidogo na shughuli nyingine za uzalishaji." Alisema Bw. Mayingu. Alisema wameamua kufanya hivyo kwa kzuingatia ukweli kuwa, katika kufuatilia wastaafu wa Mfuko wamegundua kuwa baadhi yao hujiingiza katika biashara mbalimbali ambazo hawakujiandaa vema na matokeo yake kupoteza mafao yao.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, aliongozana na Mkurugenzi wa Uendeshaji Bi. Neema Muro na Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji Bw. Gabriel Silayo, baada ya kufungwa kwa semina kwa wastaafu watarajiwa wa wilaya zote za mkoa wa Mwanza iliyofanyika ukumbi wa chuo cha watumishi wa Benki Kuu ya Tanzania, huko Capri-point jijini Mwanza. 

Bw. Mayingu, (kushoto), akijadiliana jambo na Bwana Dominic Haule, Mkurugenzi IMADS, (wakwanza kulia), wengine wanaosikiliza kutoka kushoto ni Bi. Neema Muro, Bw. Gabriel Silayo, Bw.Bw.Luseshelo Njeje na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi, baada ya kufungwa kwa semina hiyo
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, (kushoto), Mkurugezni wa Uendeshaji, Bi.Neema Muro, (katikati) na Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji, Bw. Gabriel Silayo, wakifurahia michango ya mawazo kutoka kwa washiriki wa semina.
Washiriki wakijadiliana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...