Watanzania wametakiwa kubadili fikra za kimtanzamo na kila mtu kutimiza wajibu wake kwa lengo la kuunga mkono dhamira ya serikali ya  awamu ya tano ili kujenga uchumi wa viwanda na kuboresha ustawi wa jamii.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama alisema hayo wakati alipokuwa akifungua Kongamano la Pili la  Uwezeshaji Watanzania Kiuchumi, kuwa watanzania wanatakiwa kubadili fikra za kimtanzamo ili kuweza kufikia uchumi wa viwanda, na kuboresha ustawi wa jamii.

“ Nchi yetu imeamua kubadilisha mwelekeo wa uchumi wa nchi yetu na sisi tunawajibu wa kubadili fikra za kimtanzano ili kufikia uchumi wa viwanda,” aliongeza kusema Bi. Mhagama, ambaye alifungua kongamano hilo kwa niaba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Pia aliwataka washiriki wa kongamano kwenda kushirikiana na wananchi katika kuhakikisha suala la uchumi wa wananchi unakuzwa. Na aliwasisitiza watumishi wa umma kuwa mfano katika kuchochea dhamira hiyo kwa kufanya kazi kwa vitendo.

Alisema serikali imeweka mikakati kabambe ya kuandaa nguvu kazi yenye ujuzi  inayoendana na soko la ajira kupitia program mbalimbali ikiwemo ya kuwafundisha vijana ujuzi waweze kutumika katika nguvu kazi. Na aliwataka wakuu wa mikoa yote kuainisha fursa za kiuchumi na kumpatia waziri mkuu ili zifanyiwe kazi.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama kushoto  akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Dk. John Jingu (katikati) na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo,  Bi. Beng Issa kulia wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Pili la  Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama kushoto  akikata utepe(ribbon) kuashiria kuzindua wa taarifa ya utekelezaji wa sera ya taifa ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ya Julai 2015 mpaka April 2017 wakati wa Kongamano la Pili la  Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi,(katikati) Mwenyekiti wa Bodi wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Dk. John Jingu na kulia ni  Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Bi. Beng’i Issa.  
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama kushoto  akionyesha kitabu cha taarifa ya utekelezaji wa sera ya taifa ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ya Julai 2015 mpaka April 2017 mara baada ya kuzindua taarifa hiyo wakati wa Kongamano la Pili la  Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi,(katikati) Mwenyekiti wa Bodi wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Dk. John Jingu na kulia ni  Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Bi. Beng’i Issa.  
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama kushoto  akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Bw. Joel Bendera  taarifa ya utekelezaji wa sera ya taifa ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ya Julai 2015 mpaka April 2017 mara baada ya kuzindua taarifa hiyo wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Pili la  Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC),Bi. Beng Issa.

KUSOMA ZAIDI BOPFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...