Na Mathew Kwembe, Lindi 

Jumla ya watendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa 10,931 kutoka Halmashauri 93 za Mikoa 13 inayotekeleza Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) wamepewa mafunzo ya uhasibu na utoaji wa taarifa za fedha katika awamu ya kwanza na ya pili ya mafunzo hayo yaliyofanyika katika mikoa hiyo.

Mkuu wa Mifumo ya Mawasiliano PS3 bwana Desderi Wengaa ameyasema hayo jana mjini Lindi kabla ya kumalizika kwa awamu ya pili ya mafunzo hayo ambayo yaliwahusisha waratibu wa elimu kata na waganga wafawidhi wa vituo vya afya kutoka mikoa 13 iliyo chini ya Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3).

Bwana Wengaa amefafanua kuwa katika awamu ya kwanza ya mafunzo ambayo yalitolewa kwa wakufunzi waliowafundisha watumishi kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa, jumla ya wakufunzi 2883 walipewa mafunzo hayo kwenye mikoa hiyo.

Akizungumza kabla ya kuhitimishwa kwa awamu ya pili ya mafunzo hayo yanayoendelea katika mkoa wa Lindi bwana Wengaa amesema kuwa katika awamu ya pili ya mafunzo jumla ya watumishi Mamlaka za Serikali za Mitaa 10,048 kutoka Mikoa 13 inayotekeleza Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) walifaidika na mafunzo ya uhasibu na utoaji wa taarifa za fedha.
  Mkuu wa Mifumo ya Mawasiliano PS3 bwana Desderi Wengaa akizungumza  mafanikio yaliyopatikana kwa watumishi 10931 wa Halmashauri 93 ambazo zinatekeleza Mradi wa PS3 nchini 
Baadhi ya waratibu elimu kata na waganga wafawidhi wa vituo vya afya kutoka Manispaa ya Lindi na halmashauri ya wilaya ya Lindi wakimsikiliza Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi bwana Jomaary Satura wakati alipoyafungua mafunzo hayo katika mkoa wa Lindi. 
Baadhi ya waratibu elimu kata na waganga wafawidhi wa vituo vya afya kutoka Manispaa ya Lindi na halmashauri ya wilaya ya Lindi wakimsikiliza Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi bwana Jomaary Satura wakati alipoyafungua mafunzo hayo katika mkoa wa Lindi 
Baadhi ya watoa mada ambao ni wahasibu kutoka Manispaa ya Lindi na halmashauri ya wilaya ya Lindi wakimsikiliza Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi bwana Jomaary Satura wakati alipoyafungua mafunzo hayo katika mkoa wa Lindi. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...