THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Waziri Mavunde ataka watu watumie Biko kukuza uchumi wao

NAIBU Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mheshimiwa Anthony Mavunde, amewataka Watanzania hususan wakazi na wananchi wa Dodoma kunufaika kiuchumi kwa kuutumia vyema uwapo wa mchezo wa bahati nasibu wa Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’.

Mh Mavunde ameyasema hayo jana wakati wa makabidhiano ya Sh Milioni 20 kutoka kwa mshindi wa droo ya 17 ya Biko, Evodi Mlingi, ambaye ni fundi cherehani mwenye maskani yake mjini Dodoma, akitangazwa mshindi katika droo ya 17.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Waziri Mavunde alisema kwamba serikali ya awamu ya Tano ni ya viwanda, hivyo ni jukumu la washindi hao kuhakikisha kwamba wanaanzisha na kusimamia biashara kubwa kwa kutumia mamilioni ya Biko.

Alisema fedha za Biko zinaweza kutumiwa vizuri na washindi wao, huku katika jimbo lake, mbali na watu kuibuka na ushindi wa papo kwa hapo unaonzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja zinazolipwa kwa kupitia simu za mikononi za kampuni za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money ambapo namba ya kampuni ya Biko 505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456.

“Nawataka kila mtu ahakikishe kwamba akipata fedha hizi anazitumia vizuri na mimi kama mbunge wao wa Dodoma nitasimamia katika kuwapatia mwangaza mzuri wakati wowote wakihitaji, maana lengo la serikali ni kupiga hatua kiuchumi,” Alisema.

Naye Evodi Mlingi aliwapongeza Biko kwa kuhakikisha kwamba wamemfikishia fedha zake haraka tofauti na matarajio yake, licha ya kuwa na imani kubwa na waendeshaji wa mchezo wa Biko ambao umekuwa ukitoa fedha nyingi kwa washindi wao.

“Nimekuwa mchezaji mzuri wa Biko kila siku na kila saa ambapo ninapopokea fedha ya ushindi wa papo kwa hapo naipeleka tena Biko jambo ambalo nimepata ushindi mnono kwa kuchanganya na maombi yangu kwa Mungu, maana nina uhitaji mkubwa wa fedha na hizi nilizopata naahidi kuzipeleka kwenye fungu la kumi kama nilivyotaka tangu mwanzo,” Alisema Mlingi huku akiwashauri Watanzania kucheza kwa wingi ili wapate ushindi.
Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mh Anthony Mavunde, kulia akiwa na mshindi wa droo ya 17 ya Biko, Evodi Mlingi, baada ya kukabidhiwa fedha zake jana mjini Dodoma. Waziri Mavunde amepongeza mshindi huyo na kumtaka azitumie fedha zake kwa uangalifu ili afanikiwe kiuchumi.
Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mh Anthony Mavunde kulia akiwa na wananchi wake wa Dodoma Mjini walioshinda Sh Milioni 20 za Biko kila mmoja. Evodi Mlingi katikati amekabidhiwa fedha zake jana wakati kushoto ni Ramadhan Juma Hussein aliyeshinda Milioni 20 hivi karibuni ambapo tayari ameshapokea fedha zake kutoka Biko.