* Ni la sh. milioni 213/- la fedha za maendeleo.
*Ataka apewe taarifa ifikapo Juni 30. 
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Bw. Clifford Tandari aitishe kikao na uongozi wa Halmashauri ya Kilosa na kupata kauli yao ni lini watalipa zaidi ya sh. milioni 210 wanazodaiwa na Halmashauri ya Gairo.
“Katibu Tawala itisha kikao cha Mwenyekiti wa Halmashauri, Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Halmashauri, waseme ni lini watazileta fedha hizo ambazo zilitumwa kwao wakati Halmashauri ya Wilaya ya Gairo ikiwa haijafungua akaunti zake,” amesema.
Ametoa agizo hilo jana Jumamosi, Juni 3, 2017 wakati akizungumza na viongozi wa mkoa wa Morogoro, wilaya ya Gairo na watumishi wa Halmashauri ya Gairo mara baada ya kupokea taarifa ya mkoa na wilaya katika kikao kilichofanyika Gairo mjini
“Kilosa ni lazima wazilipe hizo fedha. Katibu Tawala simamia zoezi hilo na kama watachelewa, uzikate moja kwa moja kwenye fedha yao wanayoletwa kutoka Ofisi ya Rais (TAMISEMI). Nataka nipewe taarifa ya maamuzi hayo kabla Juni haijaisha,” amesema.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi na watumishi wa Wilaya ya Gairo (hawapo pichani) katika mkutano aliouitisha mjini Gairo Juni 3, 2017.
Viongozi na watumishi wa Wilaya ya Gairo wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (hayupo pichani) katika mkutano aliouitisha mjini Gairo Juni 3, 2017. (Picha na OWM).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Bw. Cliford Tandari mara baada ya kuwasili wilayani humo (Juni 3, 2017) kwa ziara ya kikazi ya siku moja. Wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mvomero. (Picha na OWM).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipanda mti nje ya Ofisi ys Mkuu wa Wilaya ya Gairo mara baada ya kuwasili wilayani humo (Juni 3, 2017) ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Upandaji Miti Kitaifa. Wengine ni viongozi wa Mkoa na Wilaya wakishuhudia. (Picha na OWM).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimwagilia mche alioupanda nje ya Ofisi ys Mkuu wa Wilaya ya Gairo mara baada ya kuwasili wilayani humo (Juni 3, 2017) ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Upandaji Miti Kitaifa. Wengine ni viongozi wa Mkoa na Wilaya wakishuhudia. (Picha na OWM).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...