*Ni ya makontena 211 yaliyokuwa bandarini Dar
*Yabainika kuwa inafaa kwa matumizi ya kilimo
*Asisitiza wakulima waanze kupulizia mikorosho

       WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema salfa iliyoingizwa nchini kwenye makontena 211 haina kasoro na inafaa kwa matumizi ya kupulizia kwenye mikorosho.
Ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Juni 10, 2017) wakati akizungumza na wajumbe wa kamati maalum, waagizaji wa salfa na baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Korosho nchini (CBT) kwenye kikao alichokiitisha kwenye makazi yake, Oysterbay, jijini Dar es Salaam.
“Bodi kaandaeni taratibu za kawaida kusambaza salfa kwa wakulima ili waanze kupuliza dawa hiyo. Wasichelewe kupuliza kwa sababu msimu umeshaanza,” amesema.
Juni 4, mwaka huu Waziri Mkuu alimuagiza Mkemia Mkuu wa Serikali, Prof. Samuel Manyele aende kuchunguza mzigo wa salfa ulioko bandari ya Dar es Salaam baada ya kutokea mkanganyiko uliosababishwa na ripoti ya TPRI kuwa ya salfa iliyoingizwa nchini na kampuni ya ETG Inputs Ltd kwa niaba ya Bodi ya Korosho haijakidhi viwango.
  Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele akiwasilisha ripoti ya uchunguzi wa salfa kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam Juni 10, 2017. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt Mathew Mtigumwe. Kulia ni  Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti wa Ubora wa Bidhaa, Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Daniel Ndiyo  
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisikiliza ripoti ya Mkemia Mkuu wa Serikali ,  Samwel Manyele (kulia) ya chunguzi  wa Salfa  kwenye makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam Juni 10, 2017.   Wapili kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt, Mathew Mtigumwe. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...