Jumla ya Washiriki 18 kutoka mataifa mbalimbali Duniani wanatarajia kushiriki fainali ya mashindano hayo yatakayo fanyika siku ya Ijumapili Juni 18, 2017 katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es salaam.

Kwamujibu wa Mjumbe wa kamati inayo Ratibu Mashindano hayo Thabit Badi amesema mpaka sasa wameshawasili washiriki 15 na mpaka kufikia saa nane usiku kuamkia kesho watakuwa wamewasili wote.

Katika Fainali hiyo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasim Majaliwa anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi.
Washiriki wa mashindano hayo wakiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
Mjumbe wa kamati inayo ratibu Mashindano ya Qu-ran, Thabit Badi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya Mashindano ya Qu-ran yatakayofanyika siku ya Ijumapili Juni 18, mwaka huu katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...