Serikali imesema kwamba kuanzia sasa haitapeleka wagonjwa nje ya nchi kwa ajili ya kupandikiza vifaa vya usikivu kwa kuwa huduma hiyo imeanza kutolewa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Kauli hiyo imetolewa Leo na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mheshimiwa Ummy Mwalimu katika hospitali hiyo wakati akizindua huduma ya upasuaji wa kupandikiza vivaa vya usikivu (Cochlea Implant).
Ummy alisema kuwa huduma hizo zitakuwa zikitolewa Muhimbili kwa sababu ina madaktari bingwa wenye uwezo wa kufanya upasuaji huo na vifaa vya kisasa na kuokoa gharama kubwa ambazo zilikuwa zikitumika awali kupeleka wagonjwa nje ya nchi.
Waziri huyo amesema katika hospitali za umma, Tanzania imekuwa nchi ya kwanza kutoa huduma ya upandikizaji wa vifaa vya usikivu na ya pili kutoa huduma hiyo katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki ikitanguliwa na Kenya.
“Nafarijika Tanzania kuwa nchi ya kwanza kutoa huduma hii kupitia hospitali ya umma ambayo ni Muhimbili yenye hadhi ya ubingwa wa hali ya juu. Wenzetu Kenya huduma hii inatolewa kwenye hospitali binafsi na inakadiriwa kugharimu dola 31,000 za Marekani ambazi ni sawa na Sh69 milioni za Kitanzania. Hivyo basi tuna kila sababu ya kujipongeza kwa hatua tuliyofikia,”
 Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mheshimiwa Ummy Mwalimu Leo amezindua huduma mpya ya upandikizaji wa vifaa vya usikivu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH). Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi wa hospitali hiyo, Profesa Charles Majinge akifuatilie mkutano huo.
 Daktari Bingwa wa Masikio, Koo na Pua, Dkt. Edwin Liyombo wa Muhimbili akieleza jinsi mtu mwenye tatizo la kutosikia anavyofanyiwa upasuaji na kuwekea kifaa cha usikivu.
 Wataalamu walioshirikiana na madaktari na wauguzi wa Muhimbili kufanya upasuaji wa kupandikiza vifaa vya usikivu kwa watoto wakiwa kwenye mkutano huo Leo. Kutoka kulia ni Dk Sunil Dutt kutoka India, Dk Hassan Wahba wa chuo Kikuu cha Ain Shams mjini Cairo, Misri, Mohamed El Disouky anayesimamia vifaa vya usikivu Afrika na Mona Amin kutoka Kampuni ya Med-El. Wengine ni wataalamu kutoka Tanzania, Uganda na Kenya.
 Mmoja wa wazazi ambaye mtoto wake amefanyiwa upasuaji wa upandikizaji wa kifaa cha usikivu akimweleza Waziri jinsi  mtoto wake anavyozungumza vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji na kuwekewa kifaa cha usikivu.
Mama Theodora Myalla akizungumza na mheshimiwa Waziri Ummy Mwalimu baada ya mtoto wake, Mekzedeck Kibona kufanyiwa upasuaji na kuwekewa kifaa cha usikivu juzi katika Hospitali ya Muhimbili. Mtoto huyo sasa anaendelea vizuri. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...