NA HAMZA TEMBA - WMU
Wizara
ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii Tanzania TTB, imefanya
semina ya mafunzo ya siku moja kwa wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) kwa
lengo la kuwajengea uelewa wajumbe hao kuhusu majukumu ya taasisi hiyo
ambayo imefanyika jana mjini Dodoma na kuhudhuriwa na Naibu Waziri wa
Wizara hiyo, Mhandisi Ramo Makani na Katibu Mkuu, Meja Jenerali Gaudence
Milanzi.
Akizungumza
katika semina hiyo, Meneja wa Huduma za Utalii wa taasisi hiyo, Philip
Chitaunga alisema bodi hiyo iliyoanzishwa mwaka 1993 ilipewa jukumu la
jumla la kukuza sekta ya utalii nchini ikiwemo kutumia mbinu mbalimbali
za utangazaji, kuhamasisha uendelezaji wa mazao ya utalii na miundombinu
yake, kufanya tafiti za masoko na utalii kwa ujumla pamoja na
kuhamasisha uelewa wa watanzania kufahamu umuhimu na faida za utalii.
Alisema
taasisi hiyo imefanya juhudi mbalimbali za kutangaza utalii wa Tanzania
nje ya nchi ikiwemo kuratibu ziara za waandishi wa habari za kitalii,
kuweka matangazo katika magazeti ya utalii ya kimataifa, kushiriki
katika maonesho ya utalii ya kimataifa na kutangaza kupitia Televisheni
za kimataifa kama CNN ya Marekani.
“Jitihada
zingine tulizofanya ni kutumia balozi zetu nje ya nchi na mabalozi wa
utalii wa hiari yaani 'Goodwill Ambasadors', kutumia mitandao ya kijamii
na matangazo kwenye vyombo vya usafiri vya umma ambapo mwaka 2008 hadi
2009 tulitangaza kwenye mabasi 124 jijini london Uingereza, taxi 100,
treni mbalimbali na katika uwanja wa ndege wa Heathrow” alisema
Chitaunga.
Alisema
jitihada za hivi karibuni za kutangaza utalii zimefanyika kupitia
michezo ya Ligi Kuu ya Uingereza ikiwemo timu za mpira wa miguu za
Seattle Sounders na Sunderland, kupitia majarida, CD na filamu fupi kwa
lugha mbalimbali kama Kiingereza, Kijerumani, Kifaransa na Kiswahili.
Pia, kupitia tovuti maalum ya utalii ya taifa (www.tanzaniatourism.gotz),
App kwenye ‘Smart Phones’ na kufanya ziara za utangazaji wa utalii
yaani Roadshows katika nchi za China, Afrika ya Kusini, bara la Ulaya,
Amerika na Australia.
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (kushoto) akizungumza jana
mjini Dodoma katika semina iliyoandaliwa na Wizara hiyo kupitia Bodi ya Utalii
Tanzania kwa ajili ya kuwajengea uelewa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) kuhusu majukumu ya bodi hiyo. Kulia ni
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Albert Obama.
Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence
Milanzi (kushoto) akizungumza jana mjini Dodoma katika semina iliyoandaliwa na
Wizara hiyo kupitia Bodi ya Utalii Tanzania kwa ajili ya kuwajengea uelewa wajumbe
wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) kuhusu majukumu
ya bodi hiyo. Katikati ni Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani na Mwenyekiti
wa kamati hiyo, Albert Obama.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma
(PIC), Albert Obama (kulia) akizungumza jana mjini Dodoma katika semina
iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili kupitia Bodi ya Utalii Tanzania kwa ajili
ya kuwajengea uelewa wajumbe wa kamati hiyo kuhusu majukumu ya bodi hiyo. Katikati
ni Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani na Katibu Mkuu, Wizara ya
Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi.
Meneja
wa Huduma za Utalii wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Philip Chitaunga
(kushoto) akiwasilisha mada ya jumla kuhusu shughuli za taasisi hiyo kwa
wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma
(PIC) katika semina iliyoandaliwa na Wizara hiyo kupitia bodi hiyo mjini
Dodoma jana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...