Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema akimpongeza Kiongozi wa World Merit Tanzania , Rose Mmbaga katika siku ya kilele cha Mazingira Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja.

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Taasisi isiyo ya Kiserikali inayojihusisha na utunzaji wa Mazingira nchini ya Word Merit Tanzania,  imesema ipo katika kampeni maalum ya kuhakikisha kuwa Rais wa Marekani Donald Trump anatambua uwepo wa mabadiliko ya tabia nchi Duniani kwa kuanzisha kampeni ya GREEN TRUMP.

Hayo yamesemwa na kiongozi wa shirika hilo nchini Tanzania , Rose Mmbaga alipokuwa akizungumza na Ripota wa globu ya Jamii wakati wa kufunga siku ya Mazingira Duniani iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam jana.

“kwa sasa tumeamua kuwa na kampeni moja ambayo inakwenda kwa jina la ‘GREEN TRUMP’ Ambayo itawakutanisha vijana wanaojitolea kwa kupanda miti nchi nzima ili waweze kumuaminisha Rais wa Marekani kuwa mapinduzi ya kijani yanawezekana licha ya kiongozi huyu kujitoa katika ule mkataba wa Paris” amesema Mmbaga.

Ameongeza kuwa yeye kama kiongozi kijana ameamua kujikita katika kuhamasisha swala la mazingira ili kusaidia vijana wengine kuingia katika mapambano haya,ili nchi yetu iweze kujikinga na majanga mbalimbali.

Amesema kuwa mabadiliko ya tabia nchi yamekuwa yakileta majanga mengi sana nchini ikiwemo suala kurudisha maendeleo nyuma kwa kuharibu miundombinu, ambayo imejengwa kwa gharama kubwa kutoka katika fedha za watanzania.

Alimaliza kwa kusema kuwa ufike wakati wa Vijana sasa kutambua na kuheshimu mazingira ili yaweze kututunza kwa ajili ya kizazi chetu cha baadae.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema akiwa katika picha ya pamoja na Vijana wa World Merit Tanzania ambao wamejitolea kutunza Mazingira nchini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...