KAMATI za ulinzi na usalama za wilaya za Igunga,Meatu,Kishapau pamoja na Iramba zimelifunga ziwa kitangili kwa muda wa mwaka mmoja kuanzia julai,01,mwaka huu hadi Julai,01,2018 ili kulinusuru ziwa hilo lisitoweke,kulinda raslimali zilizopo na kulinda uoto wa asili ili uweze kurejea kutokana na uvuvi haramu unaoendelea katika ziwa hilo.


Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Iramba,Emmanueli Luhahula alitoa kauli hiyo kwenye mkutano wa baraza la Kawaida la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo,uliopo mjini Kiomboi.

“Lakini pia Mwenyekiti nieleze suala la ziwa Kitangili ni mwendelezo ule ule wa Mkoa wetu kuwa jangwa na sisi tuliokabidhiwa wilaya tumefanya kikao cha kamati za ulinzi na usalama wilaya nne,wilaya ya Igunga,Meatu,Kishapu na Iraamba ambao wote tunafaidika na ziwa Kitangili”alifafanua Mwenyekiti huyo.

“Utakumbuka wewe mwenyewe Mwenyekiti ulifadhili kamati hii kwenda kujadili mara ya kwanza tukiwa na baadhi ya madiwani,lakini baadaye tulikubaliana kuu zenyewe zinazosimamia ulinzi tukakutane”alisisitiza Luhahula.

Kwa mujibu wa Luhahula baada ya kukutana Mkoani Shinyanga kutokana na hali halisi ya ziwa kitangili na kutokana na tathimini ya wataalamu iliyoletwa kuhusu ziwa hilo ikieleza kwamba likiachwa jinsi lilivyo kwa kipindi cha miaka kumi ziwa hilo litakuwa limetoweka.
Baadhi ya wakuu wa idara wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo wakati wa mkutano wa kawaida wa baraza la madiwani uliofanyika mjini Kiomboi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba,Mkoani Singida,Simon Tyosela(wa kwanza kutoka kulia) akiongoza mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya hiyo.(Picha zote Na.Jumbe Ismailly).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...