THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

WADAU MBALI MBALI WA MAFUTA WAKUTANA KUJADILI ZABUNI YA UINGIZAJI WA MAFUTA KWA MWEZI WA TISA

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Serikali wa Uagizaji Mafuta ya pamoja(PBPA), Modestus Lumato akizungumza na Michuzi TV kuhusu Tenda ya Uagizaji Mafuta kwa Makampuni mbalimbali kwa Mwezi wa Tisa. Lumato amesema kuwa Uagizaji wa Mafuta hayo hufanyika mapema, kama inavyofanyika sasa mwezi wa Saba kwa Mafuta ya Mwezi wa Tisa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Zabuni ya kuagiza Mafuta kwa pamoja, Ali Saeed akifungua Sanduku la Zabuni tayari kwa kujadili Makampuni yaliyoandaa Uagizaji wa Mafuta, katika Kikao kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Zabuni ya kuingiza Mafuta kwa pamoja, Ali Saeed akiwa na bahasha za maombi tayari kwa kujadiliwa.
Baadhi ya Wawakilishi wa Makampuni yaliyoomba Zabuni ya kununua Mafuta wakiwa katika Kikao cha kupata washindi wa Zabuni hizo.