Shirika la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi nchini Tanzania limeendesha Kampeni ya Upimaji wa Maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi kwa watoto na vijana katika halmashauri ya Msalala na Manispaa ya Shinyanga katika mkoa wa Shinyanga. 

Zoezi la kupima watoto na vijana limefanyika Juni 30,2017 na Julai 1,2017 katika zanahati ya Buluma iliyopo katika kijiji cha Buuma kata ya Jana katika halmashauri ya Msalala na zanahati ya kijiji cha Galamba katika kata ya Kolandoto katika manispaa ya Shinyanga.

Zaidi ya watoto na vijana 760 walipata fursa ya kupima afya zao.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo la upimaji,Afisa Mradi, Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Shinyanga, Charles Simon, alisema kampeni ya Upimaji VVU kwa vijana na watoto yenye kauli mbiu ya “Ijue Afya ya Mwanao” inalenga kuwafikia vijana na watoto wengi zaidi ili kujua afya zao.

“Hili ni zoezi endelevu,AGPAHI kwa kushirikiana na serikali tumekuwa tukipima afya za watoto na vijana na pale inapobainika wamepata maambukizi ya VVU huwa tunawaanzishia huduma ya tiba na matunzo”,alieleza Simon.

Ijumaa Juni 30,2017: Hapa ni katika Zahanati ya Buluma iliyopo katika kijiji cha Buluma kata ya Jana halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoa wa Shinyanga .

Afisa Mradi, Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Shinyanga, Charles Simon akiwaeleza wazazi na walezi walioleta watoto na vijana katika zahanati ya Buluma kuhusu lengo la Kampeni ya Upimaji wa Maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi kwa Watoto na Vijana.

Wazazi,vijana na watoto wakimsikiliza Afisa Mradi, Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Shinyanga, Charles Simonwakati akitolea ufafanuzi juu ya kampeni ya Upimaji VVU.

Mratibu wa Wahudumu wa afya ngazi ya Jamii na Upimaji VVU wilaya ya Kahama, Peter Shimba akizungumza kabla ya zoezi la upimaji VVU halijaanza ambapo alilishukuru shirika la AGPAHI katika harakati zake za mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi na kwamba serikali itaendelea kushirikiana nalo katika mapambano hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...