Shirika la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi nchini Tanzania limekutana na waganga wakuu wa mikoa saba ambako linatekeleza shughuli zake.

AGPAHI imefanya mkutano na waganga wakuu wa mikoa ya Shinyanga,Mwanza,Geita,Simiyu,Tanga,Mara na Manyara siku ya Jumatano, Julai 5,2017 katika ukumbi wa Morena Hotel mjini Dodoma. 

 
Akizungumza katika mkutano huo,Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa alisema lengo ni kujadiliana kuhusu maendeleo, mafanikio na changamoto za miradi na kupanga mikakati ya utekelezaji wa miradi katika mwaka ujao wa miradi.

Dk. Mwakyusa alisema lengo la AGPAHI ni kuboresha afya ya watoto na familia kwa kutokomeza VVU na Ukimwi na kutoa huduma za kinga,matunzo na tiba kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa afya ikiwemo serikali ili kubuni na kutekeleza mikakati muafaka kwa afya bora.

“Shirika hili lilianzishwa mwaka 2011,kuanzia kipindi hicho tulikuwa tunafanya kazi zetu katika mikoa ya Shinyanga na Simiyu, lakini kuanzia Oktoba 2016 mikoa ya Mara,Geita,Tanga na Mwanza iliongezeka (tukitekeleza miradi ya Ukimwi) na mkoa wa Manyara uliongezeka ambako tunatekeleza mradi wa kifua kikuu”,alisema Dk. Mwakyusa.

“Tumekuwa tukifanya kazi zetu kwa kushirikiana kwa ukaribu kabisa na serikali. Na wafadhili wetu wakuu ni Watu wa Marekani kupitia shirika la Centres for Disease Control and Preventation (CDC),mfuko wa kusaidia Watoto wenye VVU kwa hisani ya Watu wa Uingereza (CIFF) na Shirika la Development Aid From People to People (ADPP - Mozambique)”, aliongeza Dk. Mwakyusa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa akielezea kuhusu miradi ya Ukimwi inayotekelezwa na shirika hilo katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania. 

 
Meneja Mawasiliano kutoka AGPAHI, Jane Shuma akiwakaribisha waganga wakuu wa mikoa katika ukumbi wa Morena Hotel mjini Dodoma kwa ajili ya kushiriki mkutano ulioandaliwa na shirika hilo. 


Waganga wakuu wa mikoa saba wakimsikiliza Dk. Mwakyusa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...