Kampuni ya simu za mkononi Airtel kwa kushirikiana na Dar Teknohama Business Incubator (DTBi) leo imezindua maabara ya Kompyuta ijulikanayo kama  ‘Airtel Fursa Lab’ katika shule ya msingi Kijitonyama iliyopo  Wilaya ya Kinondoni jijini kwa lengo la kuwawezesha vijana kupata ujuzi wa masomo.   
Akizungumza katika uzinduzi huo, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Profesa Faustine Kamuzora amesema kuwa kuweka nguvu ya pamoja kama hiyo kutawezesha kuchochea mapinduzi ya vijana wa kitanzania katika sekta ya habari na mawasiliano.  
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel, Betrice Singano amesema kuwa Airtel imejipanga kujenga vijana wenye ujuzi na weledi wakiwa bado watoto wadogo kutumia teknolojia ya mawasiliano ya simu pamoja na Tehama katika kukuza ujuzi.    
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Atamia ya Teknohama ya Dar es salaam ( DTBi) chini ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Eng. George MulaMula amesema kuwa Tanzania inachangamoto kubwa katika kutoa mafunzo kwa vitendo, hivyo maabara hiyo itachochea kasi ya ubunifu katika Teknolojia itakayoleta tija katika taifa
 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Profesa Faustine Kamuzora akizungumza katika uzinduzi maabara ya Kompyuta ijulikanayo kama  ‘Airtel Fursa Lab’ katika shule ya msingi Kijitonyama iliyopo  Wilaya ya Kinondoni leo jijini Dar es Salaam.kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Atamia ya Teknohama ya Dar es salaam ( DTBi) chini ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Eng. George MulaMula na kulia NI Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel, Betrice Singano
 Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Betrice Singano akizungumza  juu ya huduama ya maabara ya kompyuta inavyofanya kazi  kwa wanafunzi ijulikanayo kama  ‘Airtel Fursa Lab’ hafla iliyofanyika  katika shule ya msingi Kijitonyama iliyopo  Wilaya ya Kinondoni leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa Atamia ya Teknohama ya Dar es salaam ( DTBi) chini ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Eng. George MulaMula akizungumza katika hafla ya uzinduzi maabara ya Kompyuta ijulikanayo kama  ‘Airtel Fursa Lab’ katika shule ya msingi Kijitonyama iliyopo  Wilaya ya Kinondoni leo jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Profesa  Faustine Kamuzora kwakushirikiana Mkurugenzi Mkuu wa Atamia ya Teknohama ya Dar es salaam ( DTBi) chini ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Eng. George MulaMula pamoja na Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel, Betrice Singano wakikata utepe kuashiria uzinduzi  wa maabara ya Kompyuta ijulikanayo kama  ‘Airtel Fursa Lab’ katika shule ya msingi Kijitonyama iliyopo  Wilaya ya Kinondoni leo jijini Dar es Salaam
 Sehemu ya walimu na wanafunzi
 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Profesa  Faustine Kamuzora akiwa na  Mkurugenzi Mkuu wa Atamia ya Teknohama ya Dar es salaam ( DTBi) chini ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Eng. George MulaMula pamoja na Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel, Betrice Singano wakipata maelezo ya maabara ya Kompyuta ijulikanayo kama  ‘Airtel Fursa Lab’ katika shule ya msingi Kijitonyama iliyopo  Wilaya ya Kinondoni leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...