Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi (The Foundation for Civil Society- FCS), Bw. Francis Kiwanga akitoa neno la ukaribisho kwa wageni waalikwa katika Kongamano la siku moja la kuwahamasisha vijana kuchangamkia fursa za Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Kongamano hilo lilifanyika kwenye ukumbi wa Rock City Mall jijini Mwanza tarehe 19 Julai 2017. 
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mhe. Mary Onesmo Tesha ambaye alikuwa Mgeni Rasmi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongella akisoma hotuba ya ufunguzi kwenye kongmano la kuwhamasisha vijana kufanya biashara za kuvuka mipaka ya nchi za EAC. Mhe. Tesha aliwasihi vijana waondoe hofu na wajiunge katika vikundi ili waweza kufanya biashara kwa urahisi. Aliahidi kutoa milioni moja kwa kikundi kilichoundwa hapohapo kwa uratibu wa Mwkilishi wa Cloud Media, Bw. Samsonight Odera 
Bi. Tesha akiendelea na hotuba yake. 
Mchumi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw, Justin Kisoka akiwaeleza vijana wa Mwanza waliofurika kwenye ukumbi wa Rock City Mall sheria, kanuni na taratibu za kufuata kwa yeyote anayetaka kuanza biashara ya kuvuka mipaka ya nchi za EAC. 
Mtaalamu wa Msauala ya EAC, Bw. Abel Maganya akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kuhusu kufanya biashara ndani ya Jumuiya ya EAC ikiwemo namna ya kupata cheti cha uasili na hati za kusafiria. 
Mbinu mbalimbali zilitumika kufikisha ujumbe wa umuhimu wa kufanya biashara katika nchi za EAC. Hapa vijana wa Vipaji Foundation wakionesha kwa kutumia igizo baaadhi ya bidhaa zinazoweza kuuzwa katika nchi za EAC. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...