Kampuni
ya Azam Media inazindua app za kisasa kwa ajili ya habari, michezo na matangazo
ya televisheni. App
hizo za aina yake katika mifumo ya Android na iOS, zinaanza kupatika leo
Jumamosi kupitia Play Store ya Google na App Store ya Apple – unatakiwa kupakua
app yenye rangi ya njano iliyoandikwa Azam Pay TV.
Kupitia
app hizo zilizosanifiwa kwa kuzingatia mahitaji ya wateja wa ndani na nje ya
Tanzania zitakuwa na chaneli saba kwa kuanzia, ikitarajiwa chaneli nyingine
zitaendelea kuongezwa.Chaneli
hizo ni Azam One, Azam TWO, Sinema Zetu, Azam Sports HD, UTV, ZBC2 na Real
Madrid.
CEO
wa Azam Media, Tido Mhando, amesema app hizo zinatarajiwa kuleta mageuzi
makubwa katika utoaji wa huduma za televesheni na kuendana na teknolojia ya
kisasa katika soko.
“Hatua
hii tuliyofikia leo ni kielelezo tosha kuwa tunasikiliza wateja wetu wanataka
nini na tunafanya jitihada kutoa huduma zilizo bora na zenye kukidhi viwango
vinavyoendana na chapa Azam inayojulikana kote Afrika Mashariki kwa ubora,”
ameeleza Mhando.
Mhariri
wa Masuala ya Mitandao wa Azam TV, Hassan Mhelela, amesema app hizo
zimesanifiwa kuwa rahisi kuzitumia kwa kuzingatia umuhimu
wa upatikanaji wa huduma za habari na televisheni kupitia vifaa vya mkononi.
“Mfumo
huu wa Azam TV app utawawezesha watu wengi zaidi kupata taarifa na kufuatilia
vipindi vya kwenye televisheni kwa kutumia vifaa vya mkononi kama simu au
tablet. Kinachotakiwa ni mtandao wenye nguvu unaokuwezesha kucheza video au
kuangalia televisheni yaani streaming,” amesema Mhelela.
Kwa
kuanzia app hizo zinapatikana bure kwa yoyote mwenye kifaa chenye internet
kinachotumia mfumo wa Android au iOS.
Azam
Media ni kampuni tanzu ya Bakhresa Group.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...