THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

BAADA YA RATIBA YA ROBO FAINALI NDONDO CUP KUTOKA, WATANGAZAJI CLOUDS WAGAWIANA TIMU


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.


ROBO fainali ya Ndondo Cup inaendelea tena siku ya Alhamisi kwa timu nane kuumana katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo Uwanja wa Kinesi. 

Droo hiyoi iliyochezeshwa jana na kila timu kufahamu anapambana na nani katika hatua ya robo iliweza kuwa ya aina yake baada ya watangazaji wa vipindi mbalimbali wa Clouds kugawana timu hizo na kuwapa ahadi lukuki .

Hii ndo Ratiba ya Robo fainali
Alhamis 27/07/2017
Vijana Rangers vs Kibada one 
Ijumaa Tar 28/07/2017
Gomis United vs Mlalakuwa Rangers 
Jumamosi Tar 29/07/2017
Mpakani Combine vs Misosi Fc 
Jumapili Tar 30/07/2017
Keko Fanicha vs Stimutosha Fc

Kipindi cha "Leo tena" wenyewe wamebaki na timu yao Mlalakuwa Rangers, kwa hiyo hawakuwepo kwenye draw ya kila kipindi kupata timu yake. "XXL" wao timu yao ni Keko Furniture, "Jahazi" wenyewe wameangukia kwa Mpakani Kombaini, "Clouds 360" timu yao ni Misosi FC wakati "Amplifier" watakuwa na Vijana Rangers, Kibada One wameangukia kwa "Power Breakfast" huku Goms United wakitua kwa "Shilawadu" na Stim Tosha ikienda kwa wazee wa "Alasiri".
Baada ya droo hiyo kila kipindi kilitoa ahadi na mbwembwe kibao na kuziahidi timu hizo kuwa watanunua kila goli huku kipindi cha 360 wakitoa ahadi ya kuwapeleka mbuga za wanyama iwapo watakuwa mabingwa.