Baraza la ulamaa limetoa wito kwa vyombo vya dola kumchukulia hatua stahiki mtu aliyejitokeza katika mkoa wa pwani na kudai yeye ni Mtume. 

Akisoma wito huo, kwa niaba ya Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir Ally, Mwenyekiti wa Halmashauri kuu Bakwata Sheikh Hamisi Said Mataka amesema, anachodai mtu huyo aliyetajwa kwa jina la Hamza Issa kuwa yeye ni nabii hayako kabisa katika mafundisho ya kiislamu.

Amesema kauli ya Issa kudai yeye ni mtume na kisha kwamba ni Muislamu kwa kutumia maandiko ya Uislamu, ni upotoshaji mkubwa ambao ukiachwa bila kudhibitiwa ni kuruhusu fujo na uvunjifu wa amani. 

"Kwa mujibu wa maelezo yaliyoenea katika mitandao ya kijamii na ya kutoka baraza za Masheikh wa Mkoa wa Pwani chini ya kiongozi wake Sheikh na Qadhi wa Mkoa wa Pwani, amedai kuwa yeye ni Nabii Ilyasa kwa maana ya kwamba roho ya Nabii Ilyasa imemuingia yeye Hamza Issa na kwa hiyo yeye amekuwa Nabii Ilyasa" amesema Sheikh 

Ameongeza maelekezo na mafundisho ya uislamu yako wazi kuwa hakuna Mtume mwingine katika Uislamu baada ya Mtume Muhammad (S.A.W) na kwamba upatikanaji wa MTU ndani ya uislamu na kudai kuwa yeye ni Mtume ni kutaka kuamsha hisia Kali za waislamu nchini.

"Baraza la Ulamaa linapenda kuwafahamisha waislamu kwamba, yeyote atakayemfuata mpotoshaji huyu atakuwa ametoka ndani ya uislamu" amesema Sheikh Mataka. 

Pia Baraza limetoa wito kwa Masheikh wa Mikoa, Wilaya na viongozi wa taasisi mbali mbali za Kiislam kutotoa fursa ya aina yoyote kwa huyo anayejiita Nabii ( Hamza Issa), ili kuzuia kuipotosha jamii.
Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu Bakwata ,Sheikh Khamis Said akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam, juu ya Vyombo vya Dola kuchukua hatua stashiki kwa mtu mmoja mkazi wa Mkoa wa Pwani, Hamza Issa anaejiita Nabii IIyasa .
Waandishi wa Habari wakimsilikiliza Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu Bakwata, Sheikh Khamis Said, leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...